Monday, July 1, 2013

KAZA MWENDO KATIKA KAZI YA MUNGU.

Biblia inasema kwamba:

"Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani yake tu, wala si kwa mwenzake. Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe." - WAGALATIA 6:3-5.

Wapendwa; wito wetu mkuu katika Kristo Yesu ni kuhubiri Injili ya uzima ili kila aaminiye apate wokovu. Tusiridhike kwa kile kidogo tulichokifanya katika kumtumikia Mungu, bali tuzidi kukaza mwendo katika kazi ya Mungu ili neno la uzima lifike kwa watu wote. Kumbukeni nasi watakatifu tutalipwa thawabu katika uzima wa milele sawa sawa na kazi ya Mungu tuliyoifanya hapa duniani. Kama wewe ulikuwa umelala au umeridhika na kuanza kujifisu; nakukumbusha amka tena na ukaze mwendo katika kumtumikia Mungu.
Wito wetu mkuu ni kuhubiri Injili. Bwana Yesu anasema:

"
...atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?" - LUKA 18:8
Hebu tafakari haya:


Je! Kujisifu kwako, kuridhika kwako, na kujivuna kwako kuna faida gani kwa mtu asiyemjua Yesu? Je! Wewe umejiandaaje kwa ajili ya kumpokea Bwana Yesu? Je! Unafanya kazi ya kuhubiri neno la Mungu au umekufa kiroho? Ni nini wito wako basi katika Kristo? Je! Umeridhika kwa hilo ulilofanya hata umebweteka na kujisifu?


Amka, kaza mwendo kwa kuwa Mungu anataka ufanye kazi Yake kubwa kuliko hiyo uliyoifanya. Kila neno usemalo na kila tendo ufanyalo hakikisha linampa utukufu Mungu katika jina la Yesu Kristo.

0 MAONI:

Post a Comment

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii