Thursday, December 25, 2014

UKWELI KUHUSU CHIMBUKO LA SIKU KUU YA CHRISTMAS.!

UKWELI KUHUSU CHIMBUKO LA SIKU KUU YA CHRISTMAS.!


Tusiwe wanafiki, tusiwe waongo! UONGO NI DHAMBI.

Mafundisho ya Yesu kazaliwa tarehe 25 Disemba yametoka wapi? Christmas sio sikukuu ya kusheherekea tarehe ambayo Yesu amezaliwa.
Tukitazama ushahidi wa Kibiblia hauoneshi Yesu alizaliwa mwezi gani wala tarehe gani; hata pia tukitazama ushahidi wa Kihistoria nao unatubainishia kuwa Yesu Kristo alizaliwa KATIKATI YA MWAKA 6 kwenda wa 5 b.C. Hivyo basi Yesu Kristo alizaliwa miezi ya KATIKATI YA MWAKA wala sio mwishoni mwa mwaka! Mambo haya ni muhimu sana kwako Mkristo uelewe, sio unakwenda tu kama kipofu.

Kwa ushuhuda wa kweli, katika Injili zote ndani ya Biblia Takatifu hakuna mahali po pote palipoandikwa kuwa Yesu Kristo alizaliwa majira yapi wala tarehe ipi; bali tunaona tu ushuhuda wa Yesu Kristo ambaye ni Mungu aliuvaa mwili kisha akazaliwa mfano wa mwanadamu! Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kunaelezwa wazi wazi katika Injili ya Mathayo 2:1-16, na katika Injili ya Luka 2:1-7. Tangu kuzaliwa kwa Yesu, hata wakati wa utoto wa Yesu, hata wakati wa huduma ya Yesu hapa duniani, hata wakati wa mitume, hadi kufika mwaka wa 349 AD hapakuwa na sherehe ya kuzaliwa kwa Yesu mnamo tarehe 25 mwezi Disemba kila mwaka!

JE, DESTURI HII IMETOKEA WAPI?

Mara nyingi tunapoelekea mwishoni mwa kila mwaka, tangu mnamo mwaka 350 AD, watu wengi duniani husherehekea siku kuu maarufu sana ijulikanayo kwa jina Christmas. Siku kuu hiyo huadhimishwa kila tarehe 25 ya mwezi Disemba kila mwaka, na wengi huamini kuwa ndiyo tarehe ambayo Yesu Kristo alizaliwa! Je, ni kweli kuwa Yesu alizaliwa katika tarehe hiyo (tarehe 25 Disemba)?
Kusema ukweli, kabla ya mwaka 350 AD, sherehe ya Christmas haikuwepo kabisa, na wala hapakuwepo na maadhimisho ya Yesu kuzaliwa katika tarehe 25 Disemba hadi ulipofika mnamo mwaka 350 AD wakati ambao papa wa kanisa la RC aitwae jina lake Julius I alipotangaza rasmi kuwa tarehe 25 Disemba ndiyo itakuwa siku ya kusheherekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo! Julius I alifanya hivyo kwa lengo la kuifuta na kuifidia siku ambayo wapagani walikuwa wakisherehekea kuzaliwa kwa “mungu” wao JUA na mwanzo wa majira ya “Spring” (kuchipuka kwa mimea).

Katika majira hayo ayo pia kulikuwa na sikukuu ya wapagani wa Kirumi inajulikana sana kwa jina la “Roman Saturnalia” ambayo pia Warumi walikuwa wanampa heshima “mungu” wao “Saturn” (sayari ya Satan), ambaye wao walikuwa wanamwabudu kuwa ndiye “mungu” wao wa mavuno! Warumi walikuwa wanaadhimisha sherehe hiyo kila mnamo tarehe 19 ya mwezi Disemba na ilikuwa inaadhimishwa kwa siku saba mfululizo hadi tarehe 25 ya mwezi huo wa Disemba ndipo maadhimisho ya siku kuu hiyo yalipositishwa.

Vivyo hivyo, katika Ulaya kaskazini, pia nao walikuwa wanaadhimisha sherehe ijulikanayo kwa jina la “Yule” ambayo pia waliifanya kwa heshima ya “mungu” wao kwa kuwa katika majira hayo ndipo wakati ambao majira ya baridi yalikuwa wanamalizika na jua lilianza kuchomoza.

Kimsingi na kiukweli maadhimisho ya siku ya Christmas HAYAMO ki Biblia, kwa sababu hayo ni mapokeo tu yaliyowekwa na wanadamu, na tena SIO TAHERE SAHIHI ambayo Yesu Kristo alizaliwa. Ndio maana yapo mataifa yanayoadhimisha kuzaliwa kwa Yesu mnamo mwezi Januari, na mengine wanaadhimisha miezi mingine kulingana na mtazamo wao; Bali hayo maadhimisho katika tarehe 25 Disemba yametokana na fundisho la Julius I wa kanisa la RC ambaye aliliweka kulingana na mitazamo yake yeye mwenyewe; japokuwa neno “Christmas” tukilinyambua tunapata jina “Christ - Mas” ambalo maana yake inakuwa “Christ” maana yake ni “Kristo”, na “Mas” huenda likawa na maana ya “Misa” japokuwa neno “Misa” lenyewe linakuwa linaandikwa “Mass” yenye double “ss” sio single “s”!

Huo ndio ukweli kuhusu chimbuko la sherehe ya Christmas katika tarehe 25 Disemba. Kwangu mimi binafsi Christmass ipo kila siku wala sio tu tarehe 25 Disemba kwa maana kila siku kwangu ni Ibada ya Kristo, pia ninajua kwamba Yesu HAKUZALIWA MWISHONI MWA MWAKA, bali Yesu Kristo ALIZALIWA KATIKATI YA MWAKA WA 6 kwenda MWAKA WA 5 b.C.

 Uthibitisho huo wa Yesu Kristo kuzaliwa mnamo KATI KATI ya mwaka wa 6 kwenda wa 5 b.C (k.K) pia unatibitishwa na Biblia ijulikanayo kwa jina la Life Application Study Bible, katika ule ukurasa wa "A20" kama jinsi picha hii inavyoonesha katika sehemu hiyo iliyozungushishwa duara jekundu.
Na kwa takwimu hizo, hata mwaka wa kwanza A.D (b.K) Yesu Kristo tayari alikuwa na umri wa miak mitatu unusu! Na hapo pia panapingana na ile dhana inayosemwa kuwa Yesu alipozaliwa ndipo miaka ikaanza kuhesabiwa kwa mfumo wa A.D.
Hilo fundisho la Yesu kuzaliwa tarehe 25 mwezi Disemba ni uongo tupu na ni lazima tulipinge kabisa, tena Kanisa la Kristo tunatakiwa kulipinga na kulipiga vita vikali kabisa.

Tuutafuteni wokovu sio kuitafuta tarehe ambayo Yesu alizaliwa; Kila siku tunapaswa kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu na thamani ya wokovu huu; sio tu katika tarehe 25 Disemba, bali kila siku tuwe katika uwepo wa Kristo. Mimi binafsi, kila siku kwangu ni Christ mass, hata leo pia. Tarehe haiokoi, bali Yesu ndiye anaokoa.


Je, wewe unasherekeaje Christmass?

2 MAONI:

AUGUSTINO YOHANA KORONDI said...

Hapa watunwatakaa kimyaaa kiukweli,wote tunasherekea krismas sio,wakristo hadi,waislam ila ndio hivyo,Mimi,mwenyewe nilikuwa sisadiki Hilo,ila nafanya kwakuwa Ni,mazoea

Mussa Yusuph said...

Ukweli nikwamba mafundisho ya kushelehekea kikukuu yakuzaliwa Yesu ya maarufu kama bithidey. Nimoja kati yayale ambayo Yesu mwenyewe alisema kuwa watatokea manabii wakisema uwongo nakufundisha mapotofu. Wengine wakisema kristo tumemuona kule. Yesu mwenyewe amefundisha vema kuwa atakapo ondoka watakuja manabii wauongo. Nazani tumekwisha kuona mambo mengi ambayo watu wamekuwa wakifundisha ambayo Yesu akuyafanya nawala hakutuambia tufanye mojawpo yamambo ya nihaya.
1.Kuvunja amri 10 zamungu. 2.Kuazimisha kuzaliwa kwa Yesu kristo. 3.Kutoaidhini yakula vyakura najisi mfana ngurue nk. kulavyakula najisi nijambo ambalo mgunu amesema kuwa nimach ukizo lakini baadhi yamakanisa yamekuwa yakishilikiana nauyo kiongozi wakanisailo la rumi. Ukisoma biblia kwamakini unapata kuona manabii na mitume walipata tuyatolea angalizo kaba hayajafika wajijua kuwa yatatokea tu! maana mungu aliye waonyesha hayo hakuwa muongo kwao hatasikumoja. Manabii walio ya ona hayo. (1).Danieli (2).Isaya (3).Ezekieli Mitume waliyo yatazama hayo nakuyaandika (1).Mathayo (2).Marko(3).Ptro na Yohana waufunuo.Hao walijalibu kutufikishia ujumbe tusije kudanganywa Yako namengine mengi lakini katika ulimwengu wasasa tunachangamoto kubwa yakupoteza uwezo wakulielewa neno la mungu acha niseme asante napia kutufikishia uongo ambao watuwengi wanauona kuwa niukweli binafsi niekuelewa hakika mungu akubaliki amina. MUSSA YUSUPH JINALANGU NAPAIKANA KIGOMA TZ.

Post a Comment

TUMA KWA RAFIKI :

Twitter FacebookMore

 
Kuhusu Huduma Hii | Masharti Ya Utumiaji Wa Tovuti Hii | Wasiliana Nasi | Tangaza Kupitia Tovuti Hii