Imetolewa:
Mei 13, 2013
Karibu
kwenye huduma ya Neno La Uzima.
Asante kwa kutumia
huduma hii ya Neno La UZIMA. Huduma hii imeanzishwa nami Mwinjilisti Masanja C.
Sabbi. Mimi ni Mkristo niliyebatizwa kwa maji mengi na kwa Roho Mtakatifu. Ni
Mwafrika, Mtanzania ninayeishi nchi ya Tanzania (Afrika
Mashariki) katika jiji la Mwanza.
Pindi utumiapo huduma
hii, unakuwa umekubaliana na masharti yafuatayo. Tafadhari yasome kwa umakini
mkubwa sana.
Pia masharti haya yanaweza kuboreshwa kulingana na uhitaji pamoja na ulazima wa
kufanya hivyo.
Utumiapo
Tovuti Hii:
Ni lazima ufuate
masharti yote yaliyowekwa ndani ya huduma hii.
Kamwe
usiitumie vibaya huduma hii (tovuti hii). Kwa mfano,
Ø Usinakili cho chote
kilichomo ndani ya tovuti hii kwa lengo la kufanyia biashara au kujipatia
maslahi binafsi pasipo kupewa idhini ya mmiliki wa tovuti hii. Unaruhusiwa ku-“share” mafundisho haya kwa
rafiki zako (nyumbani, shuleni, chuoni, kazini, katika jamii, n.k.) kwa njia ya kusoma
moja kwa moja katika tovuti hii, au kwa njia ya kuwatumia masomo hayo kwa barua
pepe, au kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii; lakini, ni marufuku kunakili
kazi hii na kwenda kuifanyia biashara kwa namna yo yote ile.
Ø Ni marufuku kutumia
lugha ya matusi aidha kwa kutuma maoni (comment) kwenye mada
mbalimbali zilizomo ndani ya tovuti hii, au kwa ujumbe wo wote wa barua pepe,
au kwa kutumia mitandao ya kijamii, au kwa simu, wala kwa njia ya namna yo yote
ile. Endapo ukikiuka masharti haya; taratibu za kisheria zitachukua mkondo wake.
Kila mtu mtumiaji wa tovuti hii anao uhuru wa kuchangia mada yo
yote ile au kuweka maoni kwa uhuru pasipo kukiuka masharti hayo hapo juu. Pia
Biblia Takatifu inatuagiza kuyaheshimu mamlaka yaliyopo hapa duniani kwa maana
Mungu ndiye ameyaruhusu kuwepo (Warumi 13:1-7). Kuheshimu mamlaka
maana yake ni kutii kile ambacho hakipingani na neno la Mungu.
Sasa basi; kwa mujibu
wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977 toleo la mwaka 2005 (Nanukuu Katiba ya Tanzania kwa
kuwa huduma hii imeanzia katika ardhi ya Tanzania japokuwa
huduma hii ni kwa watu wote). Nanukuu baadhi ya vipengere katika “SEHEMUI YA TATU” ya Katiba hiyo
inayohusu “HAKI NA WAJIBU MUHIMU."
Nanukuu:
“Haki ya uhuru wa mtu binafsi Sheria ya 1984
Na.15 ib.6
15.-(1) Kila mtu anayo haki ya
kuwa huru na kuishi kama mtu
huru.”
“Haki ya Uhuru wa Mawazo. Uhuru wa maoni
Sheria ya 2005 Na.1 ib.5
18. Kila mtu-
(a) anao uhuru wa kuwa na
maoni na kueleza fikra zake;
(b) anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa
habari bila ya kujali mipaka ya nchi;
(c) anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya
kutoingiliwa katika mawasiliano yake; na
(d)
anayo
haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa
maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii.
19.-(1)
Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya
dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadili dini au imani yake.
(2) Kazi ya kutangaza dini,
kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi,
na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za
mamlaka ya nchi.
(3) Hifadhi ya haki zilizotajwa
katika ibara hii itakuwa chini ya taratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni
muhimu katika jamii ya kidemokrasia kwa ajili ya usalama wa jamii, amani katika
jamii, maadili ya jamii na umoja wa kitaifa.
(4) Kila palipotajwa neno “dini”
katika ibara hii ifahamike kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na
maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo
yatatafsiriwa kwa maana hiyo.”
Mwisho wa kunukuu.
Pindi
utumiapo huduma hii (Neno La UZIMA) unakuwa umekubali kutii Katiba hiyo ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kwa
mwongozo wa nukuu hizo hapo juu).
Shukurani:
Baada ya hayo; napenda kutoa shukrani za dhati kwa
kutembelea tovuti hii, na pia ninaamaini umesoma masharti hayo na umeyaelewa.
Tendo la kuendelea kutumia tovuti hii linamaanisha kuwa umekubaliana na
masharti hayo na hakika unayatekeleza.
Katika
huduma hii ya Neno la UZIMA hatubagui dini wala imani ya mtu. Upo huru
kuchangia mawazo yako pasipo kuvunja Sheria, Masharti pamoja na Taratibu
zilizowekwa.
Kumbuka
wajulishe ndugu, jamaa, na marafiki ili nao waje wajifunze neno la Mungu
kupitia huduma hii.
Ni mimi
mtumishi wa Mungu,
Mwenyezi Mungu akubariki katika jina la Yesu
Kristo, amina.