Waswahili husema kwamba: "Ukweli usioujua hauwezi kukusaidia." Nami pia nasema kwamba: "Uongo usioujua ni vigumu kuuepuka." - na: Mwinjilisti Masanja Sabbi.
Hebu soma kwa makini mafundisho haya ili upate kuifahamu iliyo kweli.
Mpenzi msomaji, bila shaka unayo shauku kubwa sana ya kujua ukweli uliojificha katika imani ya Ukristo kwani ni watu wengi tunawasikia wakijiita na kuitwa wao ni "Wakristo" lakini yawezekana wewe haujui nini hasa maana ya neno "WAKRISTO"; na pia chimbuko na asili ya imani hii. Bila shaka hapa umefungua ukurasa sahihi kabisa na utarajie kujifunza mengi na kweli tupu. Kabla hatujafika mbali katika kujifunza napenda kukupa taadhali / angalizo hili: Mara nyingi katika kujifunza unaweza ukapokea kitu kilicho kipya kwako na wakati mwingine ujumbe huu ukakuudhi kwa sababu umefichua machukizo yaliyojificha katika imani yako au dhehebu lako. Elewa kwamba; Huduma hii haipo kwa lengo la kuitukana dini au dhehebu fulani, bali dhumuni kuu la huduma hii ni kufundisha jinsi kweli ilivyo pasipo kificho.
Napenda nikushauri hivi: Lengo la kujifunza ni kutaka kujua / kuelewa kweli yote. Lakini zingatia kwamba: "Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapoikubali kweli."
Na sasa unaweza ukachukua kalamu na karatasi, au daftari ili uandike point za muhimu unazojifunza ambazo utakuwa ukijikumbushia yale uliyojifunza pindi upatapo nafasi. Baada ya utangulizi huo; napenda tujifunze kwa kina somo letu linalohusu IMANI YA UKRISTO. Hebu tuanze ifuatavyo:
IMANI YA UKRISTO
CHIMBUKO NA ASILI YA UKRISTO.
UKRISTO unatokana na neno KRISTO. Ni sawa sawa na kusema UTANZANIA unatokana na neno TANZANIA kwa sababu UTANZANIA maana yake ni utamaduni wa ki-Tanzania. Unapotamka neno KRISTO unakuwa umetamka kwa kutumia lugha ya Kiyunani (Kigiriki) lakini chimbuko na asili ya neno hilo ni neno MASIHI ambalo ni la lugha ya Kiebrania. Maneno yote hayo mawili; "KRISTO" na "MASIHI" yote yana maana moja ambayo kwa Kiswahili chepesi tafsiri yake ni Mteule wa Mungu au Mpakwa mafuta wa BWANA Mungu. Imani hii ya UPAKWA MAFUTA (UKRISTO au UMASIHI) inatokana na desturi ya Wayahudi katika nyakati za Agano la Kale hususani pindi miongoni mwao walipokuwa wanateuliwa watu kufanya kazi zifuatazo:
i/: KUHANI.
Kuhani ni mtu aliyeteuliwa na Mungu kwa ajili ya kufanya huduma ya upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. Makuhani walikuwa ni wakuu wa dini ambao kazi yao ni kuwapa watu maagizo ya Mungu au miungu yao (hata wapagani walikuwa na makuhani kwa ajili ya miungu wao. Soma Mwanzo 41:45; 47:22 hao walikuwa makuhani wa Misri) na pia makuhani walikuwa watoaji wa sadaka / kafara ambazo zimeletwa na watu kwa lengo la shukrari, au upatanisho wa dhambi zao kwa Mungu, au miungu wao.
UFAFANUZI - ZINGATIA HILI:
Watu wengine waliokuwa wanapakwa mafuta kwa ishara ya kuteuliwa na kupata kibali kwa Mungu kwa ajili ya kazi maalumu, ni hawa wafuatao:
Hiyo ndiyo chimbuko la imani ya UKRISTO, au UMASIHI, au UPAKWA MAFUTA, au UTEULE. Hadi hapo tunakuwa tumefahamu kwamba UKRISTO haukuanzia katika huduma ya Bwana Yesu kama mtu hapa duniani, bali UKRISTO ulikuwepo hata kabla ya Yesu kuja duniani kama mwanadamu. Katika nyakati za Agano la Kale huo UKRISTO au UMASIHI au UPAKWA MAFUTA au UTEULE ulikuwa wa mtu mmoja mmoja katika jamii ya Waisraeli; lakini, bado tunaona wana wa Israeli walikuwa wanatazamia kuja kwa MASIHI Mkuu yaani KRISTO Mkuu ambaye atawatawala watu wa Mungu, atakuwa kuhani kwa kufanya upatanisho, atakuwa nabii kwa kuyasema yale ayaonayo kwa YEHOVA, na pia MASIHI (yaani MTEULE) huyo atatawala milele - (Zaburi 89:3-4; Isaya 9:2-7; 11:1-5; Yeremia 23:5; Ezekieli 34:23-26; Mika 5:2) na unabii wote huo ulikuja kutimia katika Agono Jipya ambalo linamtaja wazi wazi kuwa Yesu ndiye Masihi Mkuu ambaye Yule walimtazamia atakuja - (Yohana 1:41-42). Yesu ndiye "...Mchungaji mmoja..." - (Ezekieli 34:23), ambaye ni Kuhani Mkuu - (Waebrania 7:26), na pia ndiye Masihi Mkuu - (Dan 9: 25-27). Tukisoma Biblia ya King James hapo andiko la Danieli 9:25 inamtaja Yesu kuwa ni Masihi Mwana wa Mfalme ("...Messiah the Prince...")
Sasa basi; katika nyakati hizi za Agano Jipya, imani ya UKRISTO imejengeka kutoka kwa Yesu Kristo ambaye wafuasi Wake wote amewafanya kuwa WATEULE Wake kwa kuwajaza Roho Mtakatifu ambaye ni mfano wa mafuta waliyokuwa wanapakwa wateule wa Mungu enzi za nyakati za Agano la Kale. Watu wote wamwaminio na kumtii Yesu wanaitwa WATEULE (ingekuwa ni nyakati za Agano la Kale basi nao wangemiminiwa mafuta kama ilivyokuwa desturi ya wana wa Israeli; lakini kwa sasa wanajazwa Roho Mtakatifu. Biblia inasema:
Hapo tunaona Biblia inasema: "...mafuta yale yanakaa ndani yenu..." - (1 Yohana 2:27); na pia tunaona imeandikwa: "...Roho wa Kweli... anakaa kwenu, na Yeye atakuwa ndani yenu." - (Yohana 14:17) Mafuta yale katika enzi za Agano la Kale yalitumika kama ishara tu ya kuteuliwa kwao, kwa maana imeandikwa: "...hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta..." - (1 Sam 10:1), bali kwa sasa Roho Mtakatifu Ndiye mafuta yakaayo ndani ya Wafuasi wote wa Yesu na kuwaongoza; na ndiyo ishara yetu ya kuteuliwa na Mungu, kwa maana imeandikwa: "...mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si Wake... Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu." - (Warumi 8:9, 14).
Sasa je! Ni uthibitisho upi unaotubainishia kuwa Yesu ni Masihi / Kristo? Je! YEHOVA alithibitisha hilo?
Lakini, tukizidi kutazama kwa kina imani ya Ukristo wa sasa tunaona imani hii imegawanyika katika sehemu kuu mbili, ambazo ni:
UKRISTO unatokana na neno KRISTO. Ni sawa sawa na kusema UTANZANIA unatokana na neno TANZANIA kwa sababu UTANZANIA maana yake ni utamaduni wa ki-Tanzania. Unapotamka neno KRISTO unakuwa umetamka kwa kutumia lugha ya Kiyunani (Kigiriki) lakini chimbuko na asili ya neno hilo ni neno MASIHI ambalo ni la lugha ya Kiebrania. Maneno yote hayo mawili; "KRISTO" na "MASIHI" yote yana maana moja ambayo kwa Kiswahili chepesi tafsiri yake ni Mteule wa Mungu au Mpakwa mafuta wa BWANA Mungu. Imani hii ya UPAKWA MAFUTA (UKRISTO au UMASIHI) inatokana na desturi ya Wayahudi katika nyakati za Agano la Kale hususani pindi miongoni mwao walipokuwa wanateuliwa watu kufanya kazi zifuatazo:
i/: KUHANI.
Kuhani ni mtu aliyeteuliwa na Mungu kwa ajili ya kufanya huduma ya upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. Makuhani walikuwa ni wakuu wa dini ambao kazi yao ni kuwapa watu maagizo ya Mungu au miungu yao (hata wapagani walikuwa na makuhani kwa ajili ya miungu wao. Soma Mwanzo 41:45; 47:22 hao walikuwa makuhani wa Misri) na pia makuhani walikuwa watoaji wa sadaka / kafara ambazo zimeletwa na watu kwa lengo la shukrari, au upatanisho wa dhambi zao kwa Mungu, au miungu wao.
UFAFANUZI - ZINGATIA HILI:
Utofauti kati ya "Mungu", na "mungu" - unapoandika kwa kuanza na herufi kubwa "M" yaani "Mungu" unakuwa umemtaja Mungu muumba wa vitu vyote; lakini endapo ukiandika kwa kuanza na herufi ndogo "m" yaani "mungu" hapo unakuwa umetaja "miungu" kwa maana ya watu, mizimu, pepo wachafu, au Shetani. Uwe makini sana utumiapo majina hayo. Pia uonapo katika Biblia Takatifu pameandikwa kwa herufi zote kubwa neno "BWANA" unatakiwa ujue hapo limetumiwa badala ya jina YEHOVA ambalo ndilo jina Mungu alijitambulisha kwa Musa (Kutoka 6:2,6).Hivyo basi; Mungu aliamuru makuhani wawekwe wakfu kwa kupakwa mafuta kichwani. Tunaona Mungu anamwagiza Musa kwamba:
"Nawe umlete Haruni ndugu yako karibu nami, na wanawe pamoja naye, miongoni mwa wana wa Israeli, ili anitumikie katika kazi ya ukuhani... nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia Mimi katika kazi ya ukuhani." - (Kutoka 28:1, 41)
Hapo tunaona Mungu anamwambia Musa kwamba: "...watie mafuta..." Musa alichukua mafuta na kuyatia kichwani mwao kwa ishara ya kuwa watu hao wamepewa kibali na Mungu cha kumtumikia kwa huduma ya ukuhani.
Watu wengine waliopakwa mafuta kwa ishara ya kupewa kibali na Mungu kwa kazi husika ni hawa:
ii/: WAFALME WA ISRAELI.
Tunaposoma Biblia Takatifu tunaona pia wafalme wa Israeli nao waliteuliwa kwa kupakwa mafuta matakatifu kichwani mwao. Tukimtazama mfalme Sauli tunaona Biblia inatuambia kuwa yeye ni mpakwa mafuta wa Mungu, yaani: "...masihi wa BWANA..." - (1 Sam 24:10). Wakati mfalme Sauli anawekwa wakfu, Biblia Takatifu inatuambia: "Ndipo Swamweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema,.. Nawe utawamiliki watu wa BWANA... hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta..." - (1 Sam 10:1) Pia tukija kwa mfalme Daudi tunaona naye pia alipakwa mafuta. Hapa tunaona Mungu anamwambia Samweli mtumishi Wake kwamba Samweli aende akampake Daudi mafuta ili awe mfalme wa Israeli. Tunaona Mungu anamwambia Samweli: "...Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye. Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta... na Roho ya BWANA ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile..." - (1 Sam 16:12-13) Vile vile mfalme Sulemani naye alipakwa mafuta kwa ishara ya kuteuliwa na Mungu kuwa mfalme wa Israeli. Biblia Takatifu inasema kwamba: "Na Sadoki, kuhani, akaitwaa ile pembe ya mafuta... akamtia Sulemani mafuta... Na watu wote wakasema, Mfalme Sulemani na aishi!" - (1 Wafalme 1:39) Pia tunamwona Mungu anamwambia nabii Eliya kumpaka mafuta Yehu awe mfalme wa Israeli - (1 Wafalme 19:16).Watu wengine waliokuwa wanapakwa mafuta kwa ishara ya kuteuliwa na kupata kibali kwa Mungu kwa ajili ya kazi maalumu, ni hawa wafuatao:
iii/: MANABII.
Upo wakati pia manabii nao waliteuliwa na Mungu kwa ishara ya kupakwa mafuta. Biblia Takatifu inatueleza jinsi Mungu alivyomwambia nabii Eliya kwamba:"...Elisha mwana wa Shafati wa Abel-Mehola mtie mafuta awe nabii mahali pako." - 1 Wafalme 19:16.Watu hao, yaani makuhani, wafalme wa Israeli, pamoja na manabii walikuwa wanateuliwa kwa kupakwa mafuta ambayo ni ishara ya kupata kibali mbele za Mungu kwa ajili ya kufanya kazi waliyopewa. Vile vile haikuwa tu mtu ye yote anaweza kuwapaka mafuta wateule hao, la hasha! Kazi hiyo ilifanywa na watumishi wa Mungu; nao hao watumishi hawakupaka watu ovyo ovyo bali waliongozwa na Mungu mwenyewe kwa agizo Lake. Mungu ndiye aliyechagua wateule Wake.
Hiyo ndiyo chimbuko la imani ya UKRISTO, au UMASIHI, au UPAKWA MAFUTA, au UTEULE. Hadi hapo tunakuwa tumefahamu kwamba UKRISTO haukuanzia katika huduma ya Bwana Yesu kama mtu hapa duniani, bali UKRISTO ulikuwepo hata kabla ya Yesu kuja duniani kama mwanadamu. Katika nyakati za Agano la Kale huo UKRISTO au UMASIHI au UPAKWA MAFUTA au UTEULE ulikuwa wa mtu mmoja mmoja katika jamii ya Waisraeli; lakini, bado tunaona wana wa Israeli walikuwa wanatazamia kuja kwa MASIHI Mkuu yaani KRISTO Mkuu ambaye atawatawala watu wa Mungu, atakuwa kuhani kwa kufanya upatanisho, atakuwa nabii kwa kuyasema yale ayaonayo kwa YEHOVA, na pia MASIHI (yaani MTEULE) huyo atatawala milele - (Zaburi 89:3-4; Isaya 9:2-7; 11:1-5; Yeremia 23:5; Ezekieli 34:23-26; Mika 5:2) na unabii wote huo ulikuja kutimia katika Agono Jipya ambalo linamtaja wazi wazi kuwa Yesu ndiye Masihi Mkuu ambaye Yule walimtazamia atakuja - (Yohana 1:41-42). Yesu ndiye "...Mchungaji mmoja..." - (Ezekieli 34:23), ambaye ni Kuhani Mkuu - (Waebrania 7:26), na pia ndiye Masihi Mkuu - (Dan 9: 25-27). Tukisoma Biblia ya King James hapo andiko la Danieli 9:25 inamtaja Yesu kuwa ni Masihi Mwana wa Mfalme ("...Messiah the Prince...")
Sasa basi; katika nyakati hizi za Agano Jipya, imani ya UKRISTO imejengeka kutoka kwa Yesu Kristo ambaye wafuasi Wake wote amewafanya kuwa WATEULE Wake kwa kuwajaza Roho Mtakatifu ambaye ni mfano wa mafuta waliyokuwa wanapakwa wateule wa Mungu enzi za nyakati za Agano la Kale. Watu wote wamwaminio na kumtii Yesu wanaitwa WATEULE (ingekuwa ni nyakati za Agano la Kale basi nao wangemiminiwa mafuta kama ilivyokuwa desturi ya wana wa Israeli; lakini kwa sasa wanajazwa Roho Mtakatifu. Biblia inasema:
"Nanyi, mafuta yale yanakaa ndani yenu... mafuta Yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo..." - (1 Yohana 2:27)Pia Yesu amesema: "...Yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote... na mambo yajayo atawapasha habari yake." - (Yohana 16:13) na pia Bwana Yesu amesema: "...Roho wa Kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, na Yeye atakuwa ndani yenu." - (Yohana 14:17).
Hapo tunaona Biblia inasema: "...mafuta yale yanakaa ndani yenu..." - (1 Yohana 2:27); na pia tunaona imeandikwa: "...Roho wa Kweli... anakaa kwenu, na Yeye atakuwa ndani yenu." - (Yohana 14:17) Mafuta yale katika enzi za Agano la Kale yalitumika kama ishara tu ya kuteuliwa kwao, kwa maana imeandikwa: "...hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta..." - (1 Sam 10:1), bali kwa sasa Roho Mtakatifu Ndiye mafuta yakaayo ndani ya Wafuasi wote wa Yesu na kuwaongoza; na ndiyo ishara yetu ya kuteuliwa na Mungu, kwa maana imeandikwa: "...mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si Wake... Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu." - (Warumi 8:9, 14).
Sasa je! Ni uthibitisho upi unaotubainishia kuwa Yesu ni Masihi / Kristo? Je! YEHOVA alithibitisha hilo?
Biblia Takatifu inasema kwamba:
"Alipokuwa akisema hayo, lilitokea wingu likawatia uvuli... Sauti ikatoka katika wingu, ikisema, Huyu ni Mwanangu, Mteule Wangu, msikieni Yeye." - (Luka 9:34,35)
Sauti hiyo ilikuwa ni ya YEHOVA aliyenena mbele ya Petro, Yohana na Yakobo kwa wazi kabisa kwamba YESU NDIYE MTEULE WAKE. Kumbuka kwamba; enzi za Agano la Kale, kwa wana wa Izraeli ukisema neno "Mungu" unakuwa umemtaja "YEHOVA". Hivyo ndivyo wao walivyomtambua Mwenyezi Mungu kwa jina YEHOVA - (Mwanzo 6:2; Zaburi 83:18; Isaya 26:4; Yeremia 16:21; Habakuki 3:19) Hivyo sauti hiyo ilikuwa ya YEHOVA ikimthibitisha Yesu: "...ikisema, Huyu ni Mwanangu, Mteule Wangu, msikieni Yeye." - (Luka 9:35) Imani hii ya WAKRISTO wa sasa imejengwa kutoka kwa Yesu mwenyewe ndiyo maana tunaona wafuasi Wake wanaitwa WA-KRISTO kwa maana ya kwamba "Wateule wa Yesu." Wafuasi hao wa Yesu walikuwa WATEULE tangu kabla ya watu wa mataifa kuwaita kwa jina la Wakristo - (Matendo 11:26) Bwana Yesu Mwenyewe anasema kwamba:
"Si ninyi mlionichagua Mimi, bali ni Mimi niliyewachagua ninyi..." - (Yohana 15:16)Wanafunzi wa Yesu waliteuliwa na Yesu, walijazwa Roho Mtakatifu na Yesu; hivyo walikuwa WATEULE hata kabla ya hao watu wa Antiokia kuwaita hivyo. Kwa hiyo neno MKRISTO lina maanisha "Mfuasi / Mteule wa Yesu." Ndiyo maana Biblia Takatifu inasema:
"Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili Zake Yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru Yake ya ajabu." - (1 Petro 2:9)Kila aliye mfuasi wa Yesu ameteuliwa na Mungu. Anayeteua ni Mungu wala si mwanadamu; ndiyo maana hapo tumeona pameandikwa: "...ninyi ni mzao mteule,.. taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu..." Katika nyakati za Agano la Kale kule kupakwa mafuta kichwani kulikuwa ni ishara tu - (1 Sam 10:1) ya kuteuliwa na Mungu; bali, katika nyakati hizi za Agano Jipya, kumpokea Yesu, kutii kila aliloamuru, na kujazwa Roho Mtakatifu ndiko kunakufanya uwe mteule wa Mungu - (Yohana 1:12-13). UKRISTO ni zaidi ya kupakwa mafuta, bali UKRISTO ni UTEULE. Kama jinsi ilivyokuwa katika enzi za Agano la Kale kwamba Masihi (Makristo / Wapakwa Mafuta) walikuwa ni wale tu ambao waliteuliwa na Mungu bali jamii nyingine yote walibaki kuwa ni watu wa kawaida tu; vivyo hiyo hata sasa Wakristo / Wateule ni wale tu waliompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao na kujazwa Roho Mtakatifu, hao tu peke yao ndio wateule wa Mungu - (1 Petro 2:9). Hiyo ndiyo asili ya UKRISTO na maana halisi ya imani ya UKRISTO sawa sawa na jinsi neno la Mungu lifundishavyo.
Lakini, tukizidi kutazama kwa kina imani ya Ukristo wa sasa tunaona imani hii imegawanyika katika sehemu kuu mbili, ambazo ni:
(a) Wakristo wanaosali siku ya saba ya juma (yaani Jumamosi au Saturday ya leo).
(b) Wakristo wanaosali siku ya kwanza ya juma (yaani Jumapili au Sunday ya leo).
Matabaka hayo mawili pia wanapishana katika mafundisho na mapokeo fulani fulani. Japokuwa wote wanajiita Wakristo lakini cha ajabu hawaelewani katika mafundisho yao. Waswahili husema kwamba: "Ukweli usioujua hauwezi kukusaidia." Nami pia nakwambia kwamba: "Uongo usioujua ni vigumu kuuepuka."
Je, kati ya makundi hayo mawili ya imani ya Ukristo wa sasa, ni kundi lipi linalofundisha mafundisho ya kweli sawa sawa na jinsi Yesu alivyoamuru? Yesu amesema: "...enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi... na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi..." - (Mathayo 28:18-20) Sasa, je! Ni kundi lipi kati ya hayo mawili linafundisha mafundisho ya uongo?
Kabla ya kufufika mbali katika uchambuzi huo wa kuibainisha kweli, napenda nikuulize maswali haya: Je! Unapenda kujifunza? Je! Unapenda kuifahamu kweli? Kama jibu lako ni "NDIYO" sasa basi weka kando ushabiki wa dini au dhehebu. Pia zingatia kwamba: "Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapoikubali kweli."
Katika utafiti wangu na kujifunza kwangu neno la Mungu nikiwa na watu mbalimbali, nimegundua watu wengi wanachanganywa na majina SIKU (DAYS) zilizopo kwenye juma (wiki). Ninapenda kwanza kuliweka sawa jambo hili ndipo tuendelee kujifunza kuhusu imani ya Ukristo wa sasa. Hebu kuwa makini zaidi ili uweze kuelewa vizuri.

Tunapozungumza kuhusu “siku”, katika “juma moja” (wiki moja) kuna idadi ya “siku saba”. Siku hizo zimegawanyika katika matabaka makuu “mitatu”. Naomba uwe makini ili uelewe vizuri. Matabaka hayo ndiyo yafuatavyo:
i/: KIBIBLIA. ii/: KIPAGANI, na iii/: KIISLAMU.
Inawezekana hapa ukajiuliza: Hapo unamaanisha nini? Usihofu, fatilia kwa makini nawe utanielewa vizuri.
Tukianza na siku ya JUMATATU:
i/: KIBIBLIA. ii/: KIPAGANI, na iii/: KIISLAMU.
Inawezekana hapa ukajiuliza: Hapo unamaanisha nini? Usihofu, fatilia kwa makini nawe utanielewa vizuri.
Tukianza na siku ya JUMATATU:
Kwa mujibu wa dini ya Kiislamu, kwao siku ya “Jumatatu” ya leo kwao ndiyo “siku ya tatu ya juma”. Tukilivunja vunja neno “JUMATATU” tunapata maneno mawili ambayo ni “JUMA”, na neno “TATU”. Neno “JUMA” maana yake ni “WIKI” au “muunganiko wa siku saba”, na TATU maana yake ni TATU (au THIRD - kwa Kiingereza) Kwa hiyo neno “Jumatatu” maana yake ni “siku ya tatu ya juma (wiki). Mpangilio huu umetokana na desturi ya Imani ya Kiislamu.
Tukija KIBIBLIA, siku ya “Jumatatu” ya ki-sasa ni SIKU YA PILI YA JUMA. Ambayo siku hiyo kwa upande wa WAPAGANI waanaiita MONDAY. Hao WAPAGANI siku hiyo kwao ni kwaajili ya kuabudu MWEZI (moon - kwa Kiingereza). Katika nchi za Ulaya na Asia yapo mataifa yaliyokuwa yakiabudu MWEZI (MOON). Neno MONDAY ni kifupisho cha neno MOON - DAY (Siku ya Mwezi) kwa ajili ya kumuabudu mungu wao mwezi.
Tukiingia siku ya JUMANNE:
Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, kwao JUMANNE ni SIKU YA NNE YA JUMA. Hiyo ni kutokana na desturi ya imani ya Kiislamu. Lakini tukija KIBIBLIA; siku ya JUMANNE ni siku ya TATU katika JUMA. Lakini kwa WAPAGANI wao siku ya JUMANNE wanaiita “TUESDAY”, ni siku maalumu waliyokuwa wakimuabudu mungu wao aliyejulikana kwa jina la “TIWI”. Siku hiyo wakaiita “Tiw's Day” ambayo baadae ikabadilishwa na kuitwa “TUE 's - DAY” (Siku ya Tue / Tiwi) sawa sawa na jinsi ijulikanavyo leo.
Tukiingia kwenye siku ya JUMATANO:
Kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, wao siku ya JUMATANO ni siku ya TANO katika JUMA (week - kwa Kiingereza). Kwa mujibu wa Biblia Takatifu, siku ya JUMATANO ni siku ya NNE katika JUMA (week - kwa Kiingereza). Lakini kwa WAPAGANI, siku ya JUMATANO wanaiita WEDNESDAY. Siku hiyo kwa Wapagani ni maalumu kwa kumwabudu mungu wao ajulikanae kwa jina la “WEDNE” au “WODEN” ndiyo maana siku hiyo wakaipa jina la “WEDNE 's - DAY” au kwa English nyepesi ni “Wedne ' s Day” (Siku ya Wedne) sawa sawa na jinsi ijulikanavyo leo hata nyakati za leo.
Tukiingia kwenye siku ya ALHAMISI:
Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, siku ya ALHAMISI ni siku ya SITA katika JUMA (week - kwa Kiingereza). Lakini kwa mujibu wa Biblia Takatifu, siku ya ALHAMISI ni siku ya TANO katika JUMA. Wakati huo kwa upande wa WAPAGANI, wao siku ya ALHAMISI wanaiita “THURSDAY”. Katika siku hiyo hiyo wapo WAPAGANI wanaoabudu “SAYARI YA JUPITER”, na WAPAGANI wengine ni siku maalumu kwao ya kumwabudu mungu wao aitwaye “THOR” au "THUR". Ndiyo maana siku hiyo wakaiita “THUR 's - DAY” au kwa English nyepesi ni “Thur 's Day” (Siku ya Thur).
Tukiingia kwenye siku ya IJUMAA:
Kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, siku ya IJUMAA kwao ni siku yaSABA katika JUMA (week - kwa Kiingereza). Neno IJUMAA ni neno lenye asili ya lugha ya Kiarabu likiwa na maana ya KUSANYIKO (kwa lugha ya Kiswahili). Ndiyo maana katika siku hiyo waumini ya imani ya Kiislamu hukusanyika kwenda kulitaja jina la mola wao (Allah) na kisha baada ya swala (ibada) hutawanyika kwenda kutafuta riziki zao kama jinsi kitabu cha Qur'an kinavyo waamuru. Kwao si siku ya PUMZIKO bali ni siku ya KUSANYIKO.
Kwa upande wa Biblia Takatifu, siku ya IJUMAA ni siku ya SITA katika JUMA (week - kwa Kiingereza) Lakini kwa WAPAGANI wao wanaiita FRIDAY. Kwao ni siku maalumu kwa kumwabudu mungu wao aitwaye “FRIGG” au “FREIA”. Ndiyo maana siku hiyo wakaiita FRI -DAY (Siku ya Fri).
Tukiingia kwenye siku ya JUMAMOSI:
Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, siku ya JUMAMOSI ni siku ya KANZA katika JUMA (week - kwa Kiingereza). Neno “MOSI” maana yake ni “MOJA au KWANZA ” (FIRST - kwa Kiingereza). Tumejifunza JUMA moja lina idadi ya SIKU SABA ndani yake; ndiyo maana kwa Waislamu siku ya IJUMAA tumeona ni SIKU ya SABA kwao, alafu JUMAMOSI ni SIKU ya KWANZA kwao. Hapa tunabaini kuwa hizo siku tunazozitumia Waswahili zimetokana na desturi ya mafundisho ya imani ya Kiislamu. Bila shaka hadi hapa tupo pamoja.
Tukija upande wa Biblia Takatifu; siku ya JUMAMOSI ni siku yaSABA katika JUMA. Hapa ndipo tunawapata Wakristo wenye imani ya USABATO, wao siku hiyo ni SIKU YA SABATO (PUMZIKO) kwao. Wao hupumzika siku nzima bila kufanya kazi yo yote kwa kuwa ni marufuku kwao kufanya kazi katika siku hiyo. Wasabato hiyo ni siku maalumu kwa ibada tu. Bali Wakristo wasio na imani ya Kisabato wao huendelea na kazi zao kama kawaida.
Tukija upande wa WAPAGANI, wao siku ya JUMAMOSI wameipa jina la SATURDAY. Kwao WAPAGANI ni siku maalumu ya kuabudu sayari ya SATURN. Wapo wapagani waliokuwa wanaabudu sayari ya “SATURN” ndiyo maana siku hiyo wakaipa jina la “SATUR - DAY” (yaani Siku ya Saturn).
Tukimalizia siku ya JUMAPILI:
Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu siku ya JUMAPILI kwao ni siku ya PILI katika JUMA. Lakini kwa mujibu wa Biblia Takatifu; siku ya JUMAPILI ni SIKU YAKWANZA YA JUMA. Je! Tunalitambuaje hili? Biblia Takatifu inasema:
"Hata Sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma... Yesu aliyesulibiwa... Amefufuka katika wafu..." - (Mathayo 28:1,5,7) Ndiyo maana wapo Wakristo wanaofanya ibada katika siku hiyo ya kwanza ya juma.
Tukiingia kwenye upande wa WAPAGANI siku ya JUMAPILI wao wameipa jina la “SUNDAY” yaani ni “SIKU ya JUA” (SUN). Wapo wapagani ambao wanaabudu JUA. Ndiyo maana siku hiyo wakaiita “SUN - DAY”.
Tukija KIBIBLIA, siku ya “Jumatatu” ya ki-sasa ni SIKU YA PILI YA JUMA. Ambayo siku hiyo kwa upande wa WAPAGANI waanaiita MONDAY. Hao WAPAGANI siku hiyo kwao ni kwaajili ya kuabudu MWEZI (moon - kwa Kiingereza). Katika nchi za Ulaya na Asia yapo mataifa yaliyokuwa yakiabudu MWEZI (MOON). Neno MONDAY ni kifupisho cha neno MOON - DAY (Siku ya Mwezi) kwa ajili ya kumuabudu mungu wao mwezi.
Tukiingia siku ya JUMANNE:
Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, kwao JUMANNE ni SIKU YA NNE YA JUMA. Hiyo ni kutokana na desturi ya imani ya Kiislamu. Lakini tukija KIBIBLIA; siku ya JUMANNE ni siku ya TATU katika JUMA. Lakini kwa WAPAGANI wao siku ya JUMANNE wanaiita “TUESDAY”, ni siku maalumu waliyokuwa wakimuabudu mungu wao aliyejulikana kwa jina la “TIWI”. Siku hiyo wakaiita “Tiw's Day” ambayo baadae ikabadilishwa na kuitwa “TUE 's - DAY” (Siku ya Tue / Tiwi) sawa sawa na jinsi ijulikanavyo leo.
Tukiingia kwenye siku ya JUMATANO:
Kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, wao siku ya JUMATANO ni siku ya TANO katika JUMA (week - kwa Kiingereza). Kwa mujibu wa Biblia Takatifu, siku ya JUMATANO ni siku ya NNE katika JUMA (week - kwa Kiingereza). Lakini kwa WAPAGANI, siku ya JUMATANO wanaiita WEDNESDAY. Siku hiyo kwa Wapagani ni maalumu kwa kumwabudu mungu wao ajulikanae kwa jina la “WEDNE” au “WODEN” ndiyo maana siku hiyo wakaipa jina la “WEDNE 's - DAY” au kwa English nyepesi ni “Wedne ' s Day” (Siku ya Wedne) sawa sawa na jinsi ijulikanavyo leo hata nyakati za leo.
Tukiingia kwenye siku ya ALHAMISI:
Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, siku ya ALHAMISI ni siku ya SITA katika JUMA (week - kwa Kiingereza). Lakini kwa mujibu wa Biblia Takatifu, siku ya ALHAMISI ni siku ya TANO katika JUMA. Wakati huo kwa upande wa WAPAGANI, wao siku ya ALHAMISI wanaiita “THURSDAY”. Katika siku hiyo hiyo wapo WAPAGANI wanaoabudu “SAYARI YA JUPITER”, na WAPAGANI wengine ni siku maalumu kwao ya kumwabudu mungu wao aitwaye “THOR” au "THUR". Ndiyo maana siku hiyo wakaiita “THUR 's - DAY” au kwa English nyepesi ni “Thur 's Day” (Siku ya Thur).
Tukiingia kwenye siku ya IJUMAA:
Kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, siku ya IJUMAA kwao ni siku ya
Kwa upande wa Biblia Takatifu, siku ya IJUMAA ni siku ya SITA katika JUMA (week - kwa Kiingereza) Lakini kwa WAPAGANI wao wanaiita FRIDAY. Kwao ni siku maalumu kwa kumwabudu mungu wao aitwaye “FRIGG” au “FREIA”. Ndiyo maana siku hiyo wakaiita FRI -DAY (Siku ya Fri).
Tukiingia kwenye siku ya JUMAMOSI:
Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, siku ya JUMAMOSI ni siku ya K
Tukija upande wa Biblia Takatifu; siku ya JUMAMOSI ni siku ya
Tukija upande wa WAPAGANI, wao siku ya JUMAMOSI wameipa jina la SATURDAY. Kwao WAPAGANI ni siku maalumu ya kuabudu sayari ya SATURN. Wapo wapagani waliokuwa wanaabudu sayari ya “SATURN” ndiyo maana siku hiyo wakaipa jina la “SATUR - DAY” (yaani Siku ya Saturn).
Tukimalizia siku ya JUMAPILI:
Kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu siku ya JUMAPILI kwao ni siku ya PILI katika JUMA. Lakini kwa mujibu wa Biblia Takatifu; siku ya JUMAPILI ni SIKU YA
"Hata Sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma... Yesu aliyesulibiwa... Amefufuka katika wafu..." - (Mathayo 28:1,5,7) Ndiyo maana wapo Wakristo wanaofanya ibada katika siku hiyo ya kwanza ya juma.
Tukiingia kwenye upande wa WAPAGANI siku ya JUMAPILI wao wameipa jina la “SUNDAY” yaani ni “SIKU ya JUA” (SUN). Wapo wapagani ambao wanaabudu JUA. Ndiyo maana siku hiyo wakaiita “SUN - DAY”.
Mpendwa msomaji; je! Umewahi kujiuliza kwa nini ndani ya Biblia Takatifu hakuna neno Jumatatu (Monday), Jumanne (Tuesday), Jumatano (Wednesday), Alhamisi (Thursday), Ijumaa (Friday), Jumamosi (Saturday), wala Jumapili (Sunday)? Bali utaona kwenye Biblia Takatifu pameandikwa Siku ya Kwanza, Siku ya Pili, Siku ya Tatu… Siku ya Saba? - (Mwa 1:5,8,13,19,23,31; Mathayo 28:1).
Bila shaka ufafanuzi nimeshautoa hapo juu. Hadi kufikia hapo itakuwa imeeleweka vizuri kuhusu SIKU NA MAJINA YAKE.
Sasa basi napenda moja kwa moja tujifunze kwa undani kuhusu mgawanyiko huu uliopo katika watu wa imani ya UKRISTO wa leo kwa kuanzia na WAKRISTO WENYE IMANI YA SABATO, kisha tutajifunza kuhusu WAKRISTO WANAOSALI SIKU YA KWANZA YA JUMA.
Kwa asili SABATO ilianzia pale Mungu alipomaliza kazi ya uumbaji. Biblia Takatifu inasema kwamba:
A/: WAKRISTO WENYE IMANI YA SABATO
Neno SABATO linatokana na neno la lugha ya Kiebrania liitwalo SHABBATH, au SABBATON kwa lugha ya Kiyunani, likiwa na maana ya "KUKOMA, au KUTULIA, au KUSTAREHE au PUMZIKO."Kwa asili SABATO ilianzia pale Mungu alipomaliza kazi ya uumbaji. Biblia Takatifu inasema kwamba:
"Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya." - (Mwanzo 2:2-3)
Baada ya uumbaji, kuanzia wakati wa Adamu hadi Yusufu mwana wa Yakobo (Israeli), kwa wakati huo wanadamu hawakuwa na amri ya kuiadhimisha siku ya SABATO. Kwao siku zote zilikuwa sawa. Lakini, SABATO kwa wana wa Israeli ilianzia wakati wa Musa. Biblia Takatifu inasema kwamba:
"Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, ...lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, ...wala wanyama wako.., ..wala mgeni aliye ndani ya malango yako." (Kutoka 20:8-10)Hapo Mungu anampa Musa amri ya kuikumbuka siku ya Sabato kwa kutokufanya kazi yo yote yeye wala wana wa Israeli wala wageni wo wote walio katika miji yao. Mungu alisema hivyo kwa sababu kuu mbili, nazo ni zifuatazo:
(a) Kuiweka siku hiyo kwa ajili ya kumwabudu Mungu badala ya wana wa Israeli kuitumia siku hiyo kwa kazi zao binafsi.
(b) Wapumzike kutokana na kazi walizozifanya kwa mfululizo wa siku sita ili wapate nguvu mpya itakayowaongezea ufanisi wa kufanya kazi katika siku sita nyingine zinazofuatia.
(b) Wapumzike kutokana na kazi walizozifanya kwa mfululizo wa siku sita ili wapate nguvu mpya itakayowaongezea ufanisi wa kufanya kazi katika siku sita nyingine zinazofuatia.
Kwa wana wa Israeli, siku ya Sabato iliwekwa wakfu kwa ajili ya Mungu, ilikuwa ishara kwamba watu wale waliunganishwa na Mungu kwa njia ya Agano (mapatano). Vile vile Sabato ya wana wa Israeli haikuwa Sabato ya siku tu (yaani kupumzika tu katika kila siku ya saba ya juma), bali wana wa Israeli walikuwa na SABATO YA SIKU (kupumzika siku ya saba ya kila juma,) walikuwa na MWAKA WA SABATO, na pia walikuwa na SABATO YA MASHAMBA. Sabato hizo zote zina sheria zake ambazo walilazimika kuzitekeleza.
Sabato kwa wana wa Israeli ilikuwa ni ifuatavyo:
i/: Mtu aliyefanya kazi siku hiyo alihukumiwa kifo. Ni marufuku kabisa kufanya kazi siku ya Sabato.
Kulingana na torati, ni marufuku mtu kufanya kazi yo yote katika siku ya Sabato. Endapo mtu ye yote akikiuka agizo hilo, alihukumiwa adhabu ya kifo (aliuawa). Mungu anasema kwamba:

"Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; ...Kila mtu atakayefanya kazi yo yote katika siku ya Sabato, hakika yake atauawa." - (Kutoka 31:14-15)Hayo ndiyo maneno ya Mungu Mwenyewe wala si maneno yangu mimi au ya Musa, bali ni Mungu Mwenyewe. Kwa kila mtu aliyeinajisi Sabato; hapakuwa na majadiliano wala kuomba msamaha, bali hukumu hiyo utolewa hapo hapo. Na pia kwa msisitizo neno la Mungu linasema:
"...wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangaliaHadi hapo napenda niulize swali. Je! Wasabato wa leo wanawaua watu wote wafanyao kazi yo yote katika siku ya Sabato? Je! Wasabato wa leo wanaua kila mtu anayenajisi siku ya Sabato? Je! Wasabato wa leo wanatii amri ya Mungu au wameshika mafundisho ya nani?hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele." - (Kutoka 31:16) sana
Majibu yote tutayafahamu huko mbeleni katika somo hili. Sheria nyingine ya Sabato ni hii ifuatayo:
ii/: Wanyama wote wa kufugwa watumikao katika kufanya kazi; mfano farasi, ng'ombe, punda, n.k pia nao walipaswa kupumzika siku ya Sabato. Neno la Mungu linasema kwamba:
"...siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako." - (Kutoka 20:10)Kwahiyo si wanyama tu waliopaswa kupumzika kwenye siku ya Sabato, bali pia wote hawa walitakiwa wasifanye kazi: "...wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako." Hivyo ndivyo jinsi sheria ya Sabato ilivyo.
Labda niulize swali: Je! Wasabato wa leo wanafanya hivyo?
iii/: Nchi ya mashamba, ilipumzishwa baada ya kulimwa kwa mfululizo wa miaka sita. Ule mwaka wa saba unaitwa mwaka wa Sabato kwa ajili ya mashamba. Neno la Mungu linasema kwamba:
"Panda shamba lako miaka sita, ...na kuyachuma matunda yake; lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ...usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako... Hicho kimeacho chenyewe.., usikivune, ...utakuwa mwaka wa kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi." - (Walawi 25:3-5)Hapo tunaona Mungu anasema "...mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ...usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako...utakuwa mwaka wa kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi." Niulize swali jingine tena hapa: Je! Wasabato wa leo wanafanya hivyo?
Kama jibu ni "HAWAFANYI HIVYO." Je! Nani amewapa amri ya kupunguza sheria za Mungu kwa kuchagua yale machache wayatakayo alafu wakayaboresha? Je! Huko ni kushika sheria ya Mungu au ni kushika mafundisho ya wanadamu?
Sheria nyingine ya Sabato ni hii ifuatayo:
iv/: Kuwasamehe wenye madeni wote unao wadai. Hiyo ni amri wala si hiari. Mungu anasema kwamba:
"Kila miaka saba, mwisho wake, fanya maachilio. Na jinsi ya maachilio ni hii, kila mkopeshaji na akiache alichomkopesha mwenzake, wala asimlipize mwenziwe wala nduguye; kwa kuwa imepigwa mbiu ya maachilio ya BWANA." - (Kum 15:1-2)Hapo neno "...maachilio..." limetumika kumaanisha "...samehe..." kila deni unalodai kwa ndugu yako au kwa mwenzako ye yote yule. Ndiyo maana hapo Mungu anasema: "...kila mkopeshaji na akiache alichomkopesha mwenzake, wala asimlipize mwenziwe wala nduguye..." Mbiu hiyo ya maachilio hupigwa kila mwishoni mwa miaka saba. Hapa napo tena niulize swali: Je! Wasabato wa leo wanafanya hivyo? Na pia, Sheria nyingine ya Sabato ni hii ifuatayo:
v/: Makuhani katika mwaka wa Sabato, walipaswa kuwakusanya watu wote kwa ajili ya kuwasomea sheria (Torati) hadharani, ili kuwakumbusha watu wajibu wao kwa Mungu. Masomo yale yalitekelezwa mahali rasmi pa ibada ambapo watu walikusanyika ili washerehekee sikukuu ya Vibanda.
Biblia inasema:
"Musa akaiandika torati hii, akawapa makuhani, ...na wazee wote wa Israeli. ...akawaamuru, ...Mwisho wa kila mwaka wa saba, wakati wa maachilio, wakati ulioamriwa wa sikukuu ya vibanda, ...Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni ...wapate kusikia na kujifunza, na kumcha BWANA, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii..." - (Kum 31:9-13)Biblia Takatifu inaposema "...WAPATE KUSIKIA NA KUJIFUNZA, ...NA KUANGALIA KUTENDA MANENO YOTE YA TORATI HII..." Maana yake ni kwamba kila kilichomo ndani ya torati ni lazima kukitekeleza pasipo kupunguza neno wala kuongeza neno. Je! Wasabato wa leo wanafanya hivyo?
SABATO ni amri inayopatikana ndani ya TORATI. Na pia tunapozungumzia “TORATI” maana yake ni “SHERIA” yote ambayo ndani yake tunakuta kipenyere cha Sabato. Kwa maneno ya sasa tunaweza kuifananisha TORATI na KATIBA alafu SABATO ni IBARA iliyomo ndani ya KATIBA. Biblia inalitumia neno TORATI au SHERIA kwa mtazamo mbali mbali; Upo wakati limetumiwa kwa maana ya amri au maagizo na maelezo ya jumla ambayo yametolewa na Mungu, au na wazazi, serikal, au walimu (Mwa 26:5; Kut 18:20; Zab 119:18-20, 51-61; Mhu 3:1; 6:20), mara nyingine linahusika kutaja Agano la Kale kwa ujumla, na pia mara nyingine linakuwa linataja kwa sehemu ya Agano la Kale tu hususani vile vitabu vitano vya Musa (Mt 5:17; Lk 24:44; Yn1:45; 15:25) ambavyo vilijulikana kwa jina la PENTATUKI. Jina hili "PENTATUKI" linatokana na maneno mawili ya lugha ya Kiyunani (Kigiriki) nayo ni "PENTA" maana yake ni "TANO", na neno "TEUCHOS" maana yake ni "KITABU". Waebrania waliiita PENTATUKI yote SHERIA au TORATI. Vitabu hivyo ni MWANZO (GENESIS), KUTOKA (EXODUS), WALAWI (LEVITICUS), HESABU (NUMBER) na KUMBUKUMBU LA TORATI (DEUTERONOMIUM). Hiyo ndiyo maana halisi ya TORATI au SHERIA ilivyo ki mtazamo wa Biblia.
Kwa hiyo tumeona Biblia inasema: "Musa akaiandika torati hii, akawapa makuhani, ...na wazee wote wa Israeli. ...akawaamuru, ...Mwisho wa kila mwaka wa saba, wakati wa maachilio, wakati ulioamriwa wa sikukuu ya vibanda, ...Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni ...wapate kusikia na kujifunza, na kumcha BWANA, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii..." - (Kum 31:9-13) Torati hiyo ni maagizo na amri zote zilizomo katika vitabu vyote vitano (PENTATUKI); hiyo ndiyo ambayo waliamuriwa kuishika pasipo kuongeza wala kupunguza neno lo lote lile. Pia tunaona Mungu anamwambia Musakwamba:
"Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako wapate kusikia na kujifunza, na kumcha BWANA, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii." - (Kum 31:12)Maana yake ni kwamba, wote wanalazimika kusikia, kujifunza, kumcha Mungu, na kutenda maneno yote ya hiyo sheria ambayo Musa amepewa na Mungu. Endapo ukiishi kwa kushika torati / sheria ni makosa kabisa kubagua cha kushika kulingana na matakwa yako binafsi; kwa maana imeandikwa: "Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina." - (Kum 27:26); na pia ni makosa kuongeza wala kupunguza neno lo lote lie ambalo Mungu ameamuru lifanywe. Kwa maana Mungu anasema:
"Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za BWANA, Mungu wenu, niwaamuruzo." - (Kum 4:2)Hivyo basi, Sabato ni moja kati ya amri za Mungu zilizomo ndani ya TORATI. Pia Sabato ni pana sana na inazo sheria zake kama jinsi tulivyojifunza hapo awali. Kwa maneno ya sasa tunaweza kuifananisha TORATI na KATIBA alafu SABATO ni IBARA iliyomo ndani ya KATIBA.
Kwa mara nyingine tena niulize swali; Je, Wasabato wa leo wanatekeleza yote yaliomo ndani ya torati kama jinsi Mungu alivyo amuru? Endapo kama - Hawatekelezi! JE! ASILI YA WASABATO WA LEO NI IPI?
Kumbuka Waswahili husema: "Ukweli usioujua hauwezi kukusaidia." Nami pia nasema kwamba: "Uongo usioujua ni vigumu kuuepuka." Lengo kuu la kujifunza ni kuifahamu kweli yote; Lakini zingatia kwamba: "Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapoikubali kweli."
HISTORIA YA CHIMBUKO LA WASABATO WA LEO.
Bila shaka kama umefatilia vizuri somo hili utakuwa unaelewa vizuri maana ya neno SABATO kwa mtazamo wa ki-Biblia. Sasa basi; Wasabato wa leo wanajulikana kwa jina la "Waadventista Wasabato" yaani "Seventh Day Adventists".Tofauti na Wakristo wengine:
- Wasabato wa leo (SDA) wao siku yao ya ibada ni siku ya saba ya juma (Jumamosi ya kisasa ambayo kwa mujibu wa Biblia Takatifu ndiyo siku ya saba ya juma yaani SABATO).
- Woa wanazuiwa kula baadhi ya vyakula ambavyo vinaliwa na Wakristo wa madhehebu mengine. (huko mbeleni katika somo hili tutajifunza kuhusu vyakula).
IMANI YA WASABATO WA LEO (SDA) ILIANZA KAMA IFUATAVYO:
Waasisi (waanzilishi) wa imani hiyo ni:i/: William Miller
Alizaliwa mwaka 1782 katika mji wa Pittsfield, Massachusetts, Marekani na alifariki mwaka 1849.
Alizaliwa kwenye familia ya Kikristo lakini aliuacha (aliasi imani ya Ukristo) alipokuwa kijana. Hakuiamini Biblia Takatifu kuwa ni Neno la Mungu. Katika mwaka wa 1816 aliongoka na kuurudia Ukristo, akapenda kusoma unabii kwa kina uliohusu kurudi kwa Yesu Kristo. Kutokana na kujifunza kwake unabii, alishawishika kwamba mwisho wa dunia (Kiyama) ingakuwa mwaka wa 1843. Ulipofika mwaka 1831 alitangaza hadharani maono ya unabii aliokuwanao kuhusu mwisho wa dunia. Akapata umahalufu sana sehemu nyingi na hatimaye akawa mhubiri wa dhehebu la KIBAPTISTI.
Kutokana na kwamba mwisho wa dunia unaambatana na kurudi kwa Yesu Kristo ambako kwa lugha ya Kiingereza huitwa "Christ's Advent", wafuasi wake walianza kujulikana kama "Adventists" au "Waadventista"; yaani "Watarajiao kurudi kwa Kristo."Ikumbukwe kwamba: William Miller alikuwa ni mhubiri wa dhehebu la KIBAPTIST, na hadi kufa kwake kamwe hakuwahi kuwa muumini wa dhehebu la Waadventista Wasabato (SDA) kwa sababu yeye alifariki hata kabla ya dhehebu hilo kuanzishwa; lakini mafundisho yake yamekuwa nguzo katika uasisi wa dhehebu la Waadventista Wasabato (SDA) kama jinsi tutakavyojifunza huko mbeleni katika somo hili. William Miller alikuwa ni Madventista wala si Msabato.
William Miller alishawishika kufundisha kwamba mwisho wa dunia (Kiyama) ingekuwa mwaka 1843 kutokana na jinsi yeye alivyotafsiri andiko la kitabu cha DANIELI 9:24-27. Biblia Takatifu inasema:
“Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta Yeye aliye mtakatifu. Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake Masihi aliye Mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu. Na baada ya yale majuma sitini na mawili, Masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita kuwepo; ukiwa umekwisha kusudiwa. Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.” - (Dan 9:24-27)
IFUATAYO NI TAFSIRI POTOFU YA ANDIKO LA DANIELI 9:25-27.
Tukirudi kwa upande wa William Miller: Yeye William Miller alitafsiri kule kujengwa upya kwa Yerusalemu ni pale palipoelezwa kwenye kitabu cha EZRA 7:11-26 (unaweza kusoma andiko Kisha baada ya hapo; William Miller akasoma DANIELI 8:13-14, akaona hapo kuna watakatifu wawili wakijadiliana:
"...mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi? Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa." - (Dan 8:13-14)Andiko hilo linaongelea juu ya kutakaswa kwa patakatifu kwa kipindi cha "...nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu..." Kwa hiyo William Miller akatafsiri maana ya patakatifu kutakaswa ni dunia hii iliyochafuliwa na dhambi, na utakaso huo utakuwa ndiyo hukumu (Kiyama).
Hivyo basi, kwa kutumia kanuni ile ile ya unabii ambayo siku moja ni sawa na mwaka mmoja; William Miller alichukua hizo asubuhi na jioni 2300 akazihesabu ni sawa na miaka 2300. Pia Akachukua mwaka 457 k.K akajumlisha miaka 2300 akapata mwaka wa 1843 b.K (lakini kinabii nayo hii hesabu yake inagoma, kwani ukichukua mwaka 457 k.K ukajumlisha 2300 utapata mwaka 1844 b.K kwa sababu hakuna mwaka 0 b.K). Na kwa upotofu wake yeye William Miller akaamini mwaka huo wa 1843 ndiyo ambao Yesu Kristo angerudi na ungekuwa mwisho wa dunia (Kiyama).
Ingawa mwanzoni William Miller hakutaja tarehe rasmi ya kurudi kwa Yesu, lakini baadaye alipata ujasiri wa kutangaza hadharani kwamba Yesu angerudi tarehe 21 Machi 1843. Lakini tarehe na mwaka huo ulivyopita, William Miller akabadiri tena unabii wake na akasema itakuwa tarehe 21 Machi 1844 (hapo inaonyesha alikiri kukosea hesabu yake ya awali ya kinabii.) Kinyume na jinsi vile alivyotarajia, siku hiyo nayo ilifika na kupita pasipo unabii wake kutimia. Kisha ndipo mfuasi wa karibu wa William Miller aitwaye Samweli Snow alipata ujasiri zaidi na kutangaza Yesu angerudi tarehe 22 Oktoba mwaka 1844 saa sita usiku (yeye mwenyewe anajua alipoyatoa hayo mafunuo.) Samweli Snow akasema katika siku hiyo parapanda ingepigwa, mbingu zingekunjwa kama ukaratasi, na Yesu angekuja katika utukufu mwingi. Waadventista wengi walibadili tabia zao kwa hofu ya Mungu zaidi ya zamani, baadhi ya wafanya biashara na wakulima waliuza
Zingatia neno hili, Bwana Yesu anasema kwamba:
"But of that day and hour knoweth no man, no, not the angels of heaven, but My Father only." - (Matthew 24:36 - KJV) Tafsiri yake kwa Kiswahili ni hii: "Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna mtu aijuaye, hata malaika walio mbinguni, ila Baba Yangu pekee."Mungu anasema: "Watu Wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, Mimi nami natakukataa wewe..." - (Hosea 4:6) Maarifa hayo ni neno la Mungu. Bwana Yesu amesema kwa uwazi kabisa kwamba: "Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna mtu aijuaye, hata malaika walio mbinguni, ila Baba Yangu pekee." Vile vile Biblia Takatifu inatuambia kuwa neno la Mungu la kinabii halitafsiriwi kama apendavyo mtu binafsi. Endapo kama unayo nia ya dhati kuifahamu kweli, basi zingatia kwamba: "Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapoikubali kweli."
Hivyo basi William Miller alikiri kukosea kwake, lakini akawasihi wafuasi wake wajue tu kwamba Yesu Kristo atarudi upesi. Ifahamike kwamba; hadi kufa kwake alikuwa ni Mbaptisti ambao wao wanasali siku ya kwanza ya juma (yaani Jumapili au Sunday ya kisasa) Alizaliwa mwaka 1782 b.K na kufariki mwaka 1849 b.K. Huko mbeleni tutaona jinsi mafundisho hayo ya Williamu Miller ambayo baadae yakatumiwa na Samweli Snow, na tena huko mbeleni tutaona jinsi yanavyotumika sasa kwa Waadventista Wasabato wa leo.
Mtu mwingine aliyehusika katika uanzilishi wa imani ya Waadventista Wasabato ni huyu:
ii/: Hiram Edson
Mtu huyu alikuwa mmoja kati ya wafuasi wa William Miller. Baada ya SIKU YA KUVUNJIKA MOYO, Hiram Edson pamoja na baadhi Waadventista walibaki kumwomba Mungu usiku kucha. Walimwomba Mungu awape ishara kwa nini Yesu akurudi
i/: PATAKATIFU, na ii/: PATAKATIFU PA PATAKATIFU.
Mfano wake ni kama hekalu la wana wa Israeli jinsi lilivyokuwa. Tazama picha ya mfano ufuatao (picha hii ni ya kuchora tu):
Kwa hiyo Hiram Edson akasema kwamba; siku hiyo ya tarehe 22 Oktoba 1844 saa sita usiku, Bwana Yesu Kristo alitoka sehemu inayoitwa PATAKATIFU na kuingia sehemu inayoitwa PATAKATIFU PA PATAKATIFU ndani ya hekalu la mbinguni. Kisha Yesu atabaki humo mpaka siku atakapokuja tena duniani.
Hiram Edson akasema walichokosea ndugu William Miller na Samweli Snow ni tafsiri tu. Hivyo utakaso uliofanya tangu siku hiyo si ule wa dunia hii bali ni ule wa hekalu la mbinguni ndani ya sehemu inayoitwa PATAKATIFU PA PATAKATIFU.
Kwa mujibu wa theologia ya WAADVENTISTA WASABATO, wanaamini kwamba kitu hasa ambacho Yesu Kristo anakifanya humo hekaluni tangu siku hiyo, Anafanya "INVESTIGATIVE JUDGEMENT" yaani "HUKUMU YA UPELELEZI". Wasabato wanatumia andiko la kitabu cha DANIELI 8:14 kufundishia jambohilo; imeandikwa:
i/: - William Miller alitangaza mwisho wa dunia (Kiyama) itakuwa tarehe 21 Machi 1843 (Hapa alitumia hesabu za kinabii zilizo kosewa kama jinsi tulivyojifunza huko juu.)
ii/: - William Miller alipoona siku hiyo imepita pasipo unabii wake kutimia, alighairi na kutangaza tena Kiyama kitakuwa tarehe 21 Machi 1844 (Hapa alilekebisha hesabu zake za kinabii kuitangaza tarehe hiyo kama jinsi tulivyoona hapo juu.) Nayo siku hiyo ilipita bila unabii huo kutimia.
iii/: - Samweli Snow alipata ujasiri zaidi na kutangaza Yesu angerudi tarehe 22 Oktoba mwaka 1844 saa sita usiku (Hapa ametumia hesabu za William Miller lakini yeye amebadili tarehe na mwezi bali mwaka ni ule ule.) Nayo siku hiyo ilipita bila unabii huo kutimia.
iv/: - Ndipo tunamwona Hiram Edson naye anautumia uongo uo huo kusema siku hiyo ya tarehe 22 Oktoba 1844 saa sita usiku Yesu alikuwa anaingia sehemu ya Patakatifu pa Patakatifu katika hekalu la mbinguni kufanya hukumu ya upepelezi.
Hadi hapo tumeona jinsi uongo huo ulivyokuwa unageuzwa geuzwa ili kuwaridhisha waumini wao. Zingatia neno hili, Bwana Yesu anasema kwamba:
Kabla ya kuingia katika huo ufafanuzi wa maana ya hukumu ya upelelezi (kwa mujibu wa mafundisho ya Waadventista Wasabato), hebu tazama mchoro huu hapa chini utakusaidia ili uelewe vizuri.
Ufuatao ni mchoro ambao ni mfano wa jinsi lilivyokuwa hekalu la wana wa Israeli lile lililojengwa na mfalme Sulemani.
Hiram Edson akasema walichokosea ndugu William Miller na Samweli Snow ni tafsiri tu. Hivyo utakaso uliofanya tangu siku hiyo si ule wa dunia hii bali ni ule wa hekalu la mbinguni ndani ya sehemu inayoitwa PATAKATIFU PA PATAKATIFU.
Kwa mujibu wa theologia ya WAADVENTISTA WASABATO, wanaamini kwamba kitu hasa ambacho Yesu Kristo anakifanya humo hekaluni tangu siku hiyo, Anafanya "INVESTIGATIVE JUDGEMENT" yaani "HUKUMU YA UPELELEZI". Wasabato wanatumia andiko la kitabu cha DANIELI 8:14 kufundishia jambo
"...Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa." - (Dan 8:14)Kama umefatilia kwa makini somo hili, hadi hapo utakuwa umejifunza mambo yafuatayo:
i/: - William Miller alitangaza mwisho wa dunia (Kiyama) itakuwa tarehe 21 Machi 1843 (Hapa alitumia hesabu za kinabii zilizo kosewa kama jinsi tulivyojifunza huko juu.)
ii/: - William Miller alipoona siku hiyo imepita pasipo unabii wake kutimia, alighairi na kutangaza tena Kiyama kitakuwa tarehe 21 Machi 1844 (Hapa alilekebisha hesabu zake za kinabii kuitangaza tarehe hiyo kama jinsi tulivyoona hapo juu.) Nayo siku hiyo ilipita bila unabii huo kutimia.
iii/: - Samweli Snow alipata ujasiri zaidi na kutangaza Yesu angerudi tarehe 22 Oktoba mwaka 1844 saa sita usiku (Hapa ametumia hesabu za William Miller lakini yeye amebadili tarehe na mwezi bali mwaka ni ule ule.) Nayo siku hiyo ilipita bila unabii huo kutimia.
iv/: - Ndipo tunamwona Hiram Edson naye anautumia uongo uo huo kusema siku hiyo ya tarehe 22 Oktoba 1844 saa sita usiku Yesu alikuwa anaingia sehemu ya Patakatifu pa Patakatifu katika hekalu la mbinguni kufanya hukumu ya upepelezi.
Hadi hapo tumeona jinsi uongo huo ulivyokuwa unageuzwa geuzwa ili kuwaridhisha waumini wao. Zingatia neno hili, Bwana Yesu anasema kwamba:
"But of that day and hour knoweth no man, no, not the angels of heaven, but My Father only." - (Matthew 24:36 - KJV) Tafsiri yake kwa Kiswahili ni hii: "Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna mtu aijuaye, hata malaika walio mbinguni, ila Baba Yangu pekee."Kwa hiyo tunabaini tafsiri hiyo waliyoitumia William Miller, Hiram Edson, pamoja na Samwel Snow ni tafsiri ya uongo ulio wazi kabisa. Hebu tutazame kwa kina kile wanachomaanisha kuhusu hiyo hukumu ya upelelezi:
Kabla ya kuingia katika huo ufafanuzi wa maana ya hukumu ya upelelezi (kwa mujibu wa mafundisho ya Waadventista Wasabato), hebu tazama mchoro huu hapa chini utakusaidia ili uelewe vizuri.
Ufuatao ni mchoro ambao ni mfano wa jinsi lilivyokuwa hekalu la wana wa Israeli lile lililojengwa na mfalme Sulemani.
Kama jinsi unavyoonekana huo mchoro hapo juu, itakuwa vema kwanza nikupe ufafanuzi japo kidogo kuhusu hilo hekalu.
Kwanza kabisa, ndani ya hekalu la wana wa Israeli palikuwa na sehemu mbili; Sehemu moja inaitwa "PATAKATIFU", na sehemu nyingine inaitwa PATAKATIFU PA PATAKATIFU kama jinsi uonavyo kwenye mchoro hapo juu.
Katika sehemu ile ya "PATAKATIFU" palikuwa na madhabahu, meza, pamoja na vinara kumi vya taa (vitano upande wa kushoto na vitano upande wa kulia). Sehemu hii waliruhusiwa kuingia makuhani peke yao tu. Lakini sehemu ya "PATAKATIFU PA PATAKATIFU" ilikuwa ni sehemu ya ndani zaidi ya hekalu ambamo ndani yake palikuwa na Sanduku la Agano pamoja na sanamu za Makerubi wawili. Sehemu hii aliingia kuhani mkuu peke yake tu, kuhani wa kawaida haruhusiwi kamwe kuingia humu.

Katika sehemu ya nje ya hekalu palikuwa na madhabahu ambayo makuhani walikuwa wanaitumia kwa kuteketezea dhabihu kwa ajili ya utakaso wa dhambi na maovu ya wana wa Israeli pamoja na kuteketeza dhabihu za shukrani. Mtu alipotakaswa, dhambi hizo zilihamishwa kutoka kwa mtu huyo alafu zikahamia ndani ya hekalu katika sehemu inayoitwa PATAKATIFU. Kwa kila mwaka palikuwa na siku moja ya upatanisho ambayo kuhani mkuu aliingia kulitakasa hekalu. Aliingia mahali panapoitwa PATAKATIFU PA PATAKATIFU. Alichukua mbuzi na kuweka mikono yake juu ya huyo mbuzi ndipo uovu wote na dhambi zote zilihamishiwa juu ya mbuzi huyo, kisha akachukuliwa huyo mbuzi na kwenda kuachiliwa jangwani akiwa amebeba uovu wote wa wana wa Israeli (soma WALAWI 16:20-22). Hadi hapo bila shaka utakuwa umeelewa kile kilichokuwa kinafanyika ndani ya hekalu la wana wa Israeli.
Sasa basi, fundisho la Waadventista Wasabato kuhusu hukumu ya upelelezi wanamaanisha ifuatavyo:
HUKUMU YA UPELELEZI
Kwa mujibu wa mafundisho ya Waadventista Wasabato, wao wanaamini kwamba; kabla ya Yesu Kristo kuja duniani, ipo hukumu huko mbinguni ambayo Yesu anaifanya kwakupima maisha ya Wakristo ambao majina yao yameandikwa katika KITABU CHA UZIMA. Wale ambao wanaendelea kuishi maisha matakatifu, majina yao yataendelea kubaki katika hicho KITABU CHA UZIMA, lakini wale ambao awali walikuwa wamempokea Yesu na kuishi maisha matakatifu kisha baadae wakakengeuka na kurudi nyuma kwa kuishi maisha ya dhambi, majina yao yatafutwa kutoka kwenye KITABU CHA UZIMA na kuandikwa katika KITABU CHA HUKUMU YA MAUTI YA MILELE. Hiyo ndiyo KAZI AMBAYO WASABATO WANAAMINI KWAMBA YESU KRISTO ANAIFANYA TANGU TAREHE 22 MWEZI OKTOBA MWAKA 1844 SAA SITA USIKU HADI PALE ATAKAPORUDI KWA MARA YA PILI. Kumbuka kuwa Hiram Edson ndiye aliyesema kauli hiyo baada ya Siku ya Kuvunjika Moyo (The Day of Great Disappointment) kwa sababu Yesu hakurudi tarehe 22 Oktoba 1844 kama jinsi wao walivyotarajia.
Hivyo basi; Hiram Edson akawa mtu wa kwanza aliyeleta maelezo ya kuwafariji wenzake. Ametoa mchango mkubwa sana kwenye THEOLOGIA ya WAADVENTISTA WASABATO inayohusu HUKUMU YA UPELELEZI, na mafundisho hayo yameshikwa na kuaminiwa hadi na WAADVENTISTA WASABATO wa leo, ingawa Wakristo wanaoongozwa na Maandiko Matakatifu huyaona mafundisho hayo ya WAADVENTISTA WASABATO ni UZUSHI HUSIO NA MAANA na wala hayamo ndani ya Biblia Takatifu. Hakuna andiko lo lote lile ndani ya Biblia Takatifu linalofundisha kuhusu HUKUMU YA UPELELEZI.
Mtu mwingine aliyetoa mchango wa kuanzishwa kwa imani ya Waadventista Wasabato wa leo alikuwa nihuyu afuataye:
iii/: Joseph Bates
Mtu mwingine aliyetoa mchango wa kuanzishwa kwa imani ya Waadventista Wasabato wa leo alikuwa nihuyu afuataye:
iii/: Joseph Bates
Bates alikuwa ni Mmarekani aliyeishi jimbo la Massachusetts , Marekani. Naye pia alikuwa mmoja wa viongozi maarufu wa Waadventista.
Bates baada kusoma vitabu mbalimbali kuhusu Sabato ya Wayahudi, alishawishika kuamini kwamba; siku ya Sabato, yaani JUMAMOSI, ilikuwa siku halali kwa watu wa Mungu kumwabudu Mungu.
Joseph Bates pamoja na Wabaptisti waliyokuwa wakiishi Washington, chini ya ushawishi wa Mrs. Rachel Oakes, walianzisha kundi ambalo lilikuwa la kwanza kabisa kurudia Sabato ya Agano la Kale. Bates pia akaandika kijitabu chenye kurasa 48, kilichoitwa "The Seventh Day Sabbath, a perpetual sign", pia aliandika vitabu mbalimbali kuhusu Sabato.
Anakumbukwa na WAADVENTISTA WASABATO kwa mchango mkubwa wa KUIRUDISHA SABATO YA AGANO LA KALE. Ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kutafsiri siku ya kwanza ya juma (yaani JUMAPILI au SUNDAY) kwamba ni SIKU YA ALAMA YA MNYAMA (yaani 666), na kwamba siku ya SABATO ndiyo MUHURI wa Mungu kwa watu Wake walio waaminifu. Wanatumia andiko la UFUNUO 7:4, imeandikwa:
Joseph Bates akawafundisha na kuwaaminisha kwamba hao waliotiwa mhuri ni watu 144,000 ambao waishikao Sabato.Bates baada kusoma vitabu mbalimbali kuhusu Sabato ya Wayahudi, alishawishika kuamini kwamba; siku ya Sabato, yaani JUMAMOSI, ilikuwa siku halali kwa watu wa Mungu kumwabudu Mungu.
Joseph Bates pamoja na Wabaptisti waliyokuwa wakiishi Washington, chini ya ushawishi wa Mrs. Rachel Oakes, walianzisha kundi ambalo lilikuwa la kwanza kabisa kurudia Sabato ya Agano la Kale. Bates pia akaandika kijitabu chenye kurasa 48, kilichoitwa "The Seventh Day Sabbath, a perpetual sign", pia aliandika vitabu mbalimbali kuhusu Sabato.
Anakumbukwa na WAADVENTISTA WASABATO kwa mchango mkubwa wa KUIRUDISHA SABATO YA AGANO LA KALE. Ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kutafsiri siku ya kwanza ya juma (yaani JUMAPILI au SUNDAY) kwamba ni SIKU YA ALAMA YA MNYAMA (yaani 666), na kwamba siku ya SABATO ndiyo MUHURI wa Mungu kwa watu Wake walio waaminifu. Wanatumia andiko la UFUNUO 7:4, imeandikwa:
"Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu." (UFUNUO 7:4)
WABAPTISTI wengi walivutiwa na msimamo wa Joseph Bates na kuhamua kumfuata, pamoja na watu wa madhehebu mengine mbalimbali walimfuata. Kati ya watu hao alikuwa ni James na mkewe Ellen White.
Huyo Ellen White, Wasabato wanamthamini
Ellen White amechangia kwa kiasi kikubwa
iv/: Ellen White
Jina lake kamili anaitwa Ellen Gould Harmon White, alizaliwa mwaka 1827 katika mji wa Goharm, jimbo la Maine , maili kumi toka Portland .
Kabla ya kuingia kwenye imani ya WAADVENTISTA WASABATO, Ellen White pamoja na wazazi wake walikuwa wafuasi wa kanisa la Chestnut Street Methodist.
Baada ya mwinjilisti wa KIADVENTISTA ndugu William Miller kuhubiri huko Portland katika mwaka wa 1840 na mwaka 1842, Ellen White pamoja na familia yake walivutiwa kwa mahubiri yake hususani kuhusu mwisho wa dunia, waliamua kujiunga na imani ya UADVENTISTA. Kanisa la Methodisti likaitenga familia ya Ellen White, nao tangu hapo wakawa WAADVENTISTI.
Ellen White alipokuwa MUADVENTISTI, alidai amepokea maono mengi kwa nyakati mbalimbali. Maono hayo yalimfanya atambulike kamaNABII WA WAADVENTISTA.
Maono yake ya kwanza anadai aliyapata mwezi Desemba mwaka 1844. Ellen White alidai kuwa aliyapata maono hayo kipindi kifupi tu baada ya ile siku wanayoiita "THE DAY OF GREAT DISAPPOINTMENT" yaani "SIKU YA KUVUNJIKA MOYO" ambayo ilikuwa tarehe 22 Oktoba 1844kama tulivyojifunza hapo awali. Unabii huo wa Ellen White ndio ufuatao:
Ellen White anadai kwamba: Aliona kundi la Waadventista wakisafiri katika njia yenye mwanga mkali mweupe wa utukufu, wakiongozwa na Yesu hadi walipoufikia mji wa Mungu. Alianza kutangaza na kuyahubiri maono yake hadharani mahali mbalimbali. Ilipofika tarehe 30 Agosti mwaka 1846, aliolewa na James White, ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mhubiri wa dhehebu la BAPTISTI lakini baadae akawa MUADVENTISTA.
Ulipofika mwezi Februari 1845, Ellen G. White alidai kwamba alipata maono yaliyothibitisha maono ya Hiram Edson kuhusu kile kilichotokea tarehe 22 Octoba 1844. Ellen White alidai kwamba; Yesu alikuwa ameingia katika PATAKATIFU PA PATAKATIFU ndani ya Hekalu la mbinguni.
Baada ya miaka miwili kupita; Ellen White alidai tena alipata maono ambayo alichukuliwa na kupelekwa katika Hekaluhilo la mbinguni. Kwanza kabisa, aliingizwa mahali panapoitwa PATAKATIFU, kisha baadaye akaingizwa mahali panapoitwa PATAKATIFU PA PATAKATIFU ambapo humo ndani aliona AMRI KUMI ZA MUNGU ZIKIWA NDANI YA SANDUKU LA AGANO. Akaiona ile AMRI YA NNE ambayo inahusu SABATO imezungukwa na UTUKUFU MWINGI zaidi ya amri zile nyingine tisa zilizobakia.
Maono hayo ya Ellen White, yakawa kichochezi kikibwa na nuru ya kuyaamini mafundisho kuhusu HUKUMU YA UPELELEZI na imani ya KURUDIA SABATO YA AGANO LA KALE.
Kwa ufupi hiyo ndiyo historia ya chimbuko la Waadventista Wasabato wa leo.
i/: Hiram Edson ambaye ndiye aliyeleta mafundisho kuhusu HUKUMU YA UPELELEZI wanayosadiki kwamba anaifanya Yesu Kristo tangu tarehe 22 Oktoba 1844.
ii/: Joseph Bates ambaye alisisitiza kuifuata Sabato ya Agano la Kale.
Kabla ya kuingia kwenye imani ya WAADVENTISTA WASABATO, Ellen White pamoja na wazazi wake walikuwa wafuasi wa kanisa la Chestnut Street Methodist.
Baada ya mwinjilisti wa KIADVENTISTA ndugu William Miller kuhubiri huko Portland katika mwaka wa 1840 na mwaka 1842, Ellen White pamoja na familia yake walivutiwa kwa mahubiri yake hususani kuhusu mwisho wa dunia, waliamua kujiunga na imani ya UADVENTISTA. Kanisa la Methodisti likaitenga familia ya Ellen White, nao tangu hapo wakawa WAADVENTISTI.
Ellen White alipokuwa MUADVENTISTI, alidai amepokea maono mengi kwa nyakati mbalimbali. Maono hayo yalimfanya atambulike kama
Maono yake ya kwanza anadai aliyapata mwezi Desemba mwaka 1844. Ellen White alidai kuwa aliyapata maono hayo kipindi kifupi tu baada ya ile siku wanayoiita "THE DAY OF GREAT DISAPPOINTMENT" yaani "SIKU YA KUVUNJIKA MOYO" ambayo ilikuwa tarehe 22 Oktoba 1844
Ellen White anadai kwamba: Aliona kundi la Waadventista wakisafiri katika njia yenye mwanga mkali mweupe wa utukufu, wakiongozwa na Yesu hadi walipoufikia mji wa Mungu. Alianza kutangaza na kuyahubiri maono yake hadharani mahali mbalimbali. Ilipofika tarehe 30 Agosti mwaka 1846, aliolewa na James White, ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mhubiri wa dhehebu la BAPTISTI lakini baadae akawa MUADVENTISTA.
Ulipofika mwezi Februari 1845, Ellen G. White alidai kwamba alipata maono yaliyothibitisha maono ya Hiram Edson kuhusu kile kilichotokea tarehe 22 Octoba 1844. Ellen White alidai kwamba; Yesu alikuwa ameingia katika PATAKATIFU PA PATAKATIFU ndani ya Hekalu la mbinguni.
Baada ya miaka miwili kupita; Ellen White alidai tena alipata maono ambayo alichukuliwa na kupelekwa katika Hekalu
Maono hayo ya Ellen White, yakawa kichochezi kikibwa na nuru ya kuyaamini mafundisho kuhusu HUKUMU YA UPELELEZI na imani ya KURUDIA SABATO YA AGANO LA KALE.
Kwa ufupi hiyo ndiyo historia ya chimbuko la Waadventista Wasabato wa leo.
KUANZISHWA RASMI KWA DHEHEBU LA WAADVENTISTA WASABATO (S.D.A) KULIKUWA HIVI:
Waanzilishi rasmi wa dhehebu la Waadventista Waabato (S.D.A) walikuwa ni;i/: Hiram Edson ambaye ndiye aliyeleta mafundisho kuhusu HUKUMU YA UPELELEZI wanayosadiki kwamba anaifanya Yesu Kristo tangu tarehe 22 Oktoba 1844.
ii/: Joseph Bates ambaye alisisitiza kuifuata Sabato ya Agano la Kale.
iii/: Ellen G. White ambaye Waadventista Wasabato wanamthamini
Ulipofika mwaka wa 1860, watu hao watatu wakaungana na kulipitisha jina la Seventh Day Adventist (S.D.A) na ndilo likawa jina rasmi la kundi lao, wakawa si WABAPTISTI tena. Kabla ya hapo, walikuwa ni Wabaptisti lakini walikuwa wanakutana tu kwenye jumuiya (fellowship) zao tofauti na kanisani.
Ulipowadia mwezi Mei mwaka 1863, watu hao watatu, walifanya mkutano wao mkuu wa kwanza uliokuwa na wawakilishi wa imani waliyoianzisha, kutoka majimbo yote Marekani, isipokuwa jimbo la
1. Ujio wa Yesu mara ya pili (Christ Advent) - hapo ndipo linapatikana jina Waadventista.
2. Kushika siku ya Sabato - hapo ndipo linapatikana jina Wasabato.
Hapo ndipo lilipozaliwa jina Waadventista Wasabato. Kwa ufupi hiyo ndiyo historia fupi ya jinsi imani ya Wasabato wa leo ilivyoanzishwa. Kabla hatujaendelea kujifunza, ninapenda kuuliza swali lifuatalo:
Tumejifunza na kuona jinsi Sabato ilivyokuwa inaadhimishwa na wana wa Israeli katika Agano la Kale. JE! WAADVENTISTA WASABATO WA LEO (S.D.A) WANATIMIZA YOTE YALIYOKUWA YANAFANYWA NA WAISRAELI?
"Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya..." (KUMBUKUMBU LA TORATI 27:26)Je! Waadventista Wasabato wanasemaje kuhusu andiko
"Enyi wanadamu, hata lini utukufu wangu utafedheheka? Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo?" (ZABURI 4:2)
Inasikitisha watu wameiacha kweli ambayo ni neno la Mungu na kufuata ubatili ambao ni mafundisho yaliyo kinyume na neno la Mungu. Hao wana wa Israeli hawakushika sabato peke yake, bali wao walishika TORATI yote kwa ujumla ambayo ndani ya TORATI hiyo ndimo tunaipata SABATO. Biblia Takatifu inasema kwamba:
Katika swala la Torati, ilijumuisha mambo mengi sana ikiwemo namna ya kuabudu, kazi ya makuhani, namna ya kujitakasa, hukumu mbalimbali kwa watu waliyo najisi (mfano; wakoma, na vilema walitengwa), hukumu ya papo kwa papo kwa wenye dhambi (mfano; wazinzi na wachawi walipondwa mawe hadi kufa), kushika sabato, kushika sikukuu mbalimbali, vyakula halali na najisi, pamoja na mambo mengi ambayo Mungu aliwaagiza kuyafanya. Lakini mambo hayo ni kinyume kabisa na mafundisho ya Joseph Bates, Ellen White, pamoja na Hiram Edson.
Ninapenda kusisitiza kwamba; Waisraeli si Waadventista Wasabato (S.D.A) bali Waisraeli walishika TORATI YOTE wala si Sabato peke yake, na tena Waisraeli walikuwa na dini yao ya Kiyahudi ambayo utaratibu wao wa ibada ni tofauti kabisa na Waadventista Wasabato (S.D.A). Dhehebu la Waadventista Wasabato limeanzishwa na watu watatu akiwemo Joseph Bates, Ellen White, pamoja na Hiram Edson mnamo mwezi Mei mwaka 1863.
"Mtu asiwanyang'anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili." (WAKOLOSAI 2:18)Wapo watu wanaoongozwa na maono ya mtu yatokanayo kwa akili na hisia za mtu fulani wala si neno la Mungu. Kuna watu wanaopotea kwa kuishi kwa kuongozwa na ndoto / maono / fikra badala ya kuongozwa na Mungu. Kila maono / fikra / ndoto itokayo kwa Mungu huwa na tafsiri yake na lazima haina ufunuo ulio kinyume na neno la Mungu. Napenda nikwambie neno hili: mafundisho ya wana Theolojia hayawezi kukusaidia endapo kama yapo kinyume na nano la Mungu; na pia dhehebu lako linaweza likawa kichocheo cha wewe kuingia katika hukumu ya jehanam endapo kama halitakupa mafundisho yaliyo sahihi sawa sawa na jinsi neno la Mungu lisemavyo. Ukitaka kuiponya roho yako unapaswa kuikubali kweli ambayo ni neno la Mungu. Zingatia kwamba: "Hauta elewa mpaka pale utakapo funguka akili; na hautafunguka akili mpaka pale utakapoikubali kweli."
Katika swala la Torati, ilijumuisha mambo mengi sana ikiwemo namna ya kuabudu, kazi ya makuhani, namna ya kujitakasa, hukumu mbalimbali kwa watu waliyo najisi (mfano; wakoma, na vilema walitengwa), hukumu ya papo kwa papo kwa wenye dhambi (mfano; wazinzi na wachawi walipondwa mawe hadi kufa), kushika sabato, kushika sikukuu mbalimbali, vyakula halali na najisi, pamoja na mambo mengi ambayo Mungu aliwaagiza kuyafanya. Lakini mambo hayo ni kinyume kabisa na mafundisho ya Joseph Bates, Ellen White, pamoja na Hiram Edson.
Ninapenda kusisitiza kwamba; Waisraeli si Waadventista Wasabato (S.D.A) bali Waisraeli walishika TORATI YOTE wala si Sabato peke yake, na tena Waisraeli walikuwa na dini yao ya Kiyahudi ambayo utaratibu wao wa ibada ni tofauti kabisa na Waadventista Wasabato (S.D.A). Dhehebu la Waadventista Wasabato limeanzishwa na watu watatu akiwemo Joseph Bates, Ellen White, pamoja na Hiram Edson mnamo mwezi Mei mwaka 1863.
SOMO HILI BADO LINAENDELEA; LITAKUWA HEWANI PUNDE. MWENDELEZO WAKE UTAKUWEPO HAPA HAPA KATIKA UKURASA HUU.
Endelea kujifunza masomo mengine mazuri yaliyomo katika huduma hii.
Mwenyezi Mungu akubariki kwa kufungua ukurasa huu.