SOMO: - MSAMAHA
Tukisoma kitabu cha WAEFESO 4:31,32 tunaona Biblia
Takatifu inasema kwamba:
"Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele
na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili
ninyi kwa ninyi, wenye huruma, MKASAMEHEANE kama
na Mungu katika Kristo ALIVYOWASAMEHE ninyi." (Efe 4:31,32)
Je! Nini maana ya neno MSAMAHA na kuna faida zipi
katika KUSAMEHE; na kwa nini
tunapaswa KUSAMEHE?
MSAMAHA:
Neno “MSAMAHA” ni neno
jepesi kulitamka lakini ni pana sana
katika maana. Nisemapo "NI NENO JEPESI KULITAMKA" ninamaanisha
kulitamka tu kwa kawaida na katika hali ya kawaida tu pasipo kukosewa, lakini
kwa watu wengi; neno MSAMAHA ni neno gumu sana
kulitamka toka rohoni mwao hususani pindi wanapokosewa. Nilifanya utafiti juu
ya hili neno nikagundua zipo siri kubwa sana
katika KUSAMEHE ambazo Shetani apendi watu wazifahamu.
Tukirudi kwenye neno “SAMEHE” maana yake ni: Kukoma / kuacha kuhisi hasira juu ya mtu ambaye amekuumiza, kakukwaza au kakuudhi; Pia, kukoma / kuacha kuhisi hasira juu yako wewe mwenyewe (kuto kujichukia).
Neno MSAMAHA, kwa maana nyepesi linamaanishakama
ifuatavyo;
Tukirudi kwenye neno “SAMEHE” maana yake ni: Kukoma / kuacha kuhisi hasira juu ya mtu ambaye amekuumiza, kakukwaza au kakuudhi; Pia, kukoma / kuacha kuhisi hasira juu yako wewe mwenyewe (kuto kujichukia).
Neno MSAMAHA, kwa maana nyepesi linamaanisha
Þ
Kutolipiza
kisasi japokuwa unayo haki ya kulipiza kisasi.
Þ
Ni tendo la
imani na tena la hiari kwa kuwa unayo sababu, uwezo, na haki ya kulipiza kisasi
kutokana na yale uliyo umizwa.
Je! Unafahamu ni kwa nini
watu wengi ni wagumu KUSAMEHE?
Watu wengi hushindwa
kusamehe kwa sababu hawana Roho Mtakatifu ndani yao ;
kwamba, wameruhusu maisha yao
kutawaliwa na Shetani.
Dhana hiyo inao ukweli mkubwa ndani yake na pia wapo watu wajiitao watumishi wa Mungu lakini nao wanashindwa KUSAMEHE. Si kwamba tu tunasamehe ili na sisi tupate kusamehewa; La, si hivyo tu, bali zipo faida nyingisana zipatikanazo kwenye KUSAMEHE.
Siku zote mtu anapokosewa, ndani yake anazaa UCHUNGU, asipokuwa makini nao UCHUNGU unazaa CHUKI, na pia hasipojiadhari hiyo CHUKI inazaa HASIRA. Na hapo ndipo Shetani anapata mlango wa kumwingia mtu. Vitu hivyo vitatu; yaani, UCHUNGU, CHUKI na HASIRA mara zote huandamana. Usipoweza kuudhibiti UCHUNGU, unakuwa unaweka wazi mlango wa Shetani kukutawala.
Mtu kuokoka haimaanishi ndiyo mwisho wa makwazo na majaribu mbalimbali, bali tambua unapo mpokea Yesu Kristo awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako unakuwa umetangaza vita dhidi ya Shetani na majeshi yake ya pepo waovu. Shetani atajaribu kukuingia moja kwa moja, lakini akishindwa, anatafuta mbinu ya kumuingia mtu mwingine ili akukwaze; nawe ukikwazika ndipo Shetani anapata nafasi ya kukuingia na kukutawala kupitia UCHUNGU, CHUKI, na HASIRA.
Tumeona mifano mingi ya watumishi wa Mungu walio anguka kiimani kwa kushindwa KUSAMEHE; Huduma nyingi za kuhubiri Neno la Mungu zimekufa kwasababu ya KUTOSAMEHE; Makanisa mengi yamevunjika na kutengana kwa sababu tu ya KUTOSAMEHE; Ndoa nyingi na uchumba mwingi umevunjika kwasababu ya KUTOSAMEHE; Makampuni mengi yamevunjika kwa sababu ya KUTOKUSAMEHE, utaona mkurugenzi amekwazana na meneja alafu kampuni inapoteza muelekeo, utendaji unakuwa mbovu na hatimae kampuni inakufa. Yote hayo unaweza kukuta chanzo chake ni KUTOSAMEHE.
Siku zote unapokwazika Shetani anakuwa anakuletea hati ya mashtaka kwenye mawazo yako; utasikia siuti ikikwambia;
Dhana hiyo inao ukweli mkubwa ndani yake na pia wapo watu wajiitao watumishi wa Mungu lakini nao wanashindwa KUSAMEHE. Si kwamba tu tunasamehe ili na sisi tupate kusamehewa; La, si hivyo tu, bali zipo faida nyingi
Siku zote mtu anapokosewa, ndani yake anazaa UCHUNGU, asipokuwa makini nao UCHUNGU unazaa CHUKI, na pia hasipojiadhari hiyo CHUKI inazaa HASIRA. Na hapo ndipo Shetani anapata mlango wa kumwingia mtu. Vitu hivyo vitatu; yaani, UCHUNGU, CHUKI na HASIRA mara zote huandamana. Usipoweza kuudhibiti UCHUNGU, unakuwa unaweka wazi mlango wa Shetani kukutawala.
Mtu kuokoka haimaanishi ndiyo mwisho wa makwazo na majaribu mbalimbali, bali tambua unapo mpokea Yesu Kristo awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako unakuwa umetangaza vita dhidi ya Shetani na majeshi yake ya pepo waovu. Shetani atajaribu kukuingia moja kwa moja, lakini akishindwa, anatafuta mbinu ya kumuingia mtu mwingine ili akukwaze; nawe ukikwazika ndipo Shetani anapata nafasi ya kukuingia na kukutawala kupitia UCHUNGU, CHUKI, na HASIRA.
Tumeona mifano mingi ya watumishi wa Mungu walio anguka kiimani kwa kushindwa KUSAMEHE; Huduma nyingi za kuhubiri Neno la Mungu zimekufa kwasababu ya KUTOSAMEHE; Makanisa mengi yamevunjika na kutengana kwa sababu tu ya KUTOSAMEHE; Ndoa nyingi na uchumba mwingi umevunjika kwasababu ya KUTOSAMEHE; Makampuni mengi yamevunjika kwa sababu ya KUTOKUSAMEHE, utaona mkurugenzi amekwazana na meneja alafu kampuni inapoteza muelekeo, utendaji unakuwa mbovu na hatimae kampuni inakufa. Yote hayo unaweza kukuta chanzo chake ni KUTOSAMEHE.
Siku zote unapokwazika Shetani anakuwa anakuletea hati ya mashtaka kwenye mawazo yako; utasikia siuti ikikwambia;
"YAANI FULANI
AKUFANYIE HIVI KABISA ALAFU UMSAMEHE? HAPANA !!! LAZIMA UMKOMESHE. HAIWEZEKANI
UMSAMEHE HIVI HIVI TU WAKATI AMEKUPA HASARA YOTE HII.”
Ndipo nawe waweza ukajikuta yanakuingia
akilini na ukaanza kusema: “Kweli; HAIWEZEKANI KABISA, TENA YAANI, ATANITAMBUA
MIMI NI NANI."
Utaona Shetani
anakukumbushia tukio jinsi ulivyo tendewa. Utasikia ushauri mwingi sana ndani ya fahamu zako.
Tena maneno hayo yanaweza kukupa UCHUNGU sana
kiasi cha kushindwa kula, na hata ukatokwa na machozi. Na akili ya mwanadamu ni
rahisi kunasa mabaya kuliko mema; ni rahisi kukumbuka mabaya kuliko mema; hapo
ndipo Shetani huchukulia point endapo usipokuwa makini. Ukimruhusu Shetani
katika akili zako; ndipo utajikuta ukimtazama aliyekukwaza ni mtu wa karibu sana nawe, ambae ulitegemea angekuwa msaada kwako lakini
amekurudisha nyuma na kuuumiza sana
moyo wako. Hauna raha, amani wala matumaini yoyote yale. Yawezekana akawa ni
rafiki yako wa karibu sana
amesababisha ufukuze kazi kwa kosa ambalo hukulifanya. Kweli inauma sana ; inaleta huzuni na
uchungu ukiwaza utafanya nini na wale wanaokutegemea. Inaumiza sana .
Kwa wakati huo, ukijitizama uwezo wa kumdhuru unao, sababu ya kumdhuru unayo, na nia ya kumdhuru unayo. Na kila mtu unaemsimulia anakwambia:
Kwa wakati huo, ukijitizama uwezo wa kumdhuru unao, sababu ya kumdhuru unayo, na nia ya kumdhuru unayo. Na kila mtu unaemsimulia anakwambia:
"Mbona wewe mjinga
hivyo? Ingekuwa ni mimi, kamwe siwezi kumlazia damu huyo, lazima
angenitambua."
Kwa wakati huo moyo wako
umejaa UCHUNGU, CHUKI na HASIRA. Lakini kwa mbali saaaana, unasikia sauti ndani
ya moyo wako ikisema: MSAMEHE.
Nadhani ata wewe waweza kutambua ni jinsi gani ilivyo vigumu kuitii hiyo sauti isemayo SAMEHE kwa kuwa ukitazama ni kweli umeonewa, uwezo wa kulipa kisasi unao, na hata ukilipa kisasi au kudhuru wapo watu watakaosema "Kwa kweli umefanya vizuri kumkomesha. Ilimpasa hivyo."
Nakama ukitenda jambo baya juu yake; fahamu
kwamba hiyo imetokana na wewe kuruhusu UCHUNGU ukutawale. Wengine hufikia hata
hatua ya kujinyonga. Mawazo yatakujia; “Yaani fulani kabisa azini na mke wangu
! Tena fulani ni rafiki yangu kabisa ! Hapana. Lazima nimkomeshe.”
Nadhani ata wewe waweza kutambua ni jinsi gani ilivyo vigumu kuitii hiyo sauti isemayo SAMEHE kwa kuwa ukitazama ni kweli umeonewa, uwezo wa kulipa kisasi unao, na hata ukilipa kisasi au kudhuru wapo watu watakaosema "Kwa kweli umefanya vizuri kumkomesha. Ilimpasa hivyo."
Na
Hayo yote chanzo chake ni
UCHUNU uliouruhusu uingie ndani ya nafsi (akili) yako. Tumeona Biblia Takatifu
inatuambia kwamba: "Uchungu wote na ghadhabu na hasira
na kelele na matukano yaondoke kwenu..." (Efe 4:31) Sasa; je! Nini maana ya neno UCHUNGU? Nivigumu
kupambana na adui kama hatumfahamu adui yetu
UCHUNGU ni nani.
Kwa maana nyepesi neno
UCHUNGU maana yake ni hii:
Þ
Ni hali ya
kutokuwa na furaha, kujawa hasira zilizotokana na kutendewa mabaya.
Þ
Ni hali ya
kuhisi huzuni nzito ambayo wakati mwingine inaweza kuchangamana na maumivu
makali katika fahamu za mtu, ambayo yaweza kusababisha mwili kunyong'onyea na
kusababisha akili kupoteza uwezo wa kufikiri vizuri.
Mara nyingi UCHUNGU
husababisha akili kushindwa kufanya kazi ipasavyo. Hiyo ndiyo maana halisi ya
neno uchungu. Zifuatazo
ni athali za kutosamehe;
i/: KUHARIBU AFYA YAKO.
Uchungu unapomwingia
Pia, UCHUNGU husababisha
mtu kuwa na mawazo yenye maswali yasiyo na majibu kwa wepesi; na tena tumaini
huonekana kama vile limepotea kabisa. Uchungu
huo ukidumu kwa muda mrefu husababisha mwili kutengeneza sumu itakayoharibu ule
ute mwepesi unaopatikana katikati ya mifupa (Synovial fluid) pamoja na kuharibu
afya yako kwa ujumla (Bila shaka hapa madaktari wananielewa vizuri.) UCHUNGU huo
ukizidi kupita kiasi, mwili wa mtu huyo huonekana umekakamaa kakamaa sana . Na kwa kiasi kikubwa
afya ya mtu huyu huanza kuharibika hatua baada ya hatua. Mwili wake
hunyong'onyea na akili zake hushindwa kufanya kazi vizuri, hupoteza kumbukumbu
na utambuzi wa mambo mbali mbali na kumfanya mtu afanye maamuzi ya pupa
yanayompeleka kwenye hasara kubwa zaidi badala ya kuleta suluhu la matatizo
yake.
ii/: KUTENGWA NA WATU.
KUTOKUSAMEHE kunasababisha
GHADHABU na HASIRA. Na hivi vyote hutokea pale unaposhindwa KUUDHIBITI UCHUNGU
USIKUTAWALE. Mlango mkubwa wa DHAMBI huanzia pale mtu anaposhindwa kudhibiti
UCHUNGU. Kwa hiyo; UCHUNGU unapomtawala mtu, uchungu huo unazaa kitu
kinachoitwa CHUKI. Ndani ya hii chuki ndimo kunakaa GHADHABU. GHADHABU ni hali
ya mtu kuwa na maamuzi ya pupa pasipo kujali madhara yake. Hali hiyo yaweza
kumfanya mtu kuwa na majibu ya mkato mkato, kutopenda kuulizwa ulizwa; humfanya
mtu kuwa na hali ya UGOMVI mara kwa mara, kutopenda kuwa na subira (anataka
afanyiwe vitu kwa haraka haraka la sivyo ananuna na kutoa maneno machafu, na
wakati mwingine anakuwa na tabia ya kuzira). Katika hatua hii ndipo kunazaliwa
kitu kiitwacho HASIRA. HASIRA umfanya mtu kuchukua maamuzi pasipo kujali. Mtu
huyo kwa wakati huo anakuwa hatarini sana
kuingiliwa na Shetani. Endapo asipodhibiti hiyo hasira yawezekana Shetani
akamwendesha kama jinsi Shetani apendavyo.
Hapo ndipo utaona MAGOMVI, MATUSI na KILA AINA YA UBAYA vinadhihirika kwa mtu
huyo. Tena anafanya pasipo hata kujali. Mtu hukirihusu hasira ikutawale utakuwa
umempa Shetani kibali cha kukutawala. Biblia Takatifu inasema kwamba:
"Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira
nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na
kujipatia nafsi yako mtego." (MITHALI 22:24-25).
Mtego huo hutoka kwa Shetani ili akuingize
dhambini. Hivyo basi; matokeo ya
hasira ni KUTENGWA NA WATU. Kwa kuwa mtu huyo hufanya maamuzi bila kutumia
akili, hekima wala busara.
Neno la Mungu linapotuambia:
"UCHUNGU WOTE NA GHADHABU NA HASIRA NA KELELE NA MATUKANO YAONDOKE KWENU,
PAMOJA NA KILA NAMNA YA UBAYA.." Mungu anatutaka vitu hivyo viondoke kwetu
kwa ajili ya faida yetu wenyewe. Lakini ukishindwa kuvidhibiti, matokeo yake
utafikia hatua itakayokupa hasara kimwili na kiroho pia. Na ufahamu kwamba; MTU
KUSHINDWA KUDHIBITI UCHUNGU USIMTAWALE kunaweza kuwa CHANZO CHA MABAYA NA
DHAMBI KUTOKEA. Ndiyo maana utaweza kuona mtu amegombana na mke wake nyumbani
alafu anaondoka na hasira zake kisha unasikia amegongwa na gari barabarani.
Sasa jiulize, kusamehe ni kwa ajili ya faida kwa Mungu au kwako wewe mwenyewe?
Au yawezekana umedhurumiwa pesa zako na wafanya biashara wenzako kisha ukaingia
ofisini mwako umejaa hasira, wateja wanapokuja wewe unawajibu vibaya; Je,
biashara yako ikifa utamlaumu Mungu, Shetani au lawama ni juu yako wewe
uliyeshindwa KUZUIA HUO UCHUNGU? Dawa ya kuushinda uchungu ni KUSAMEHE; hakuna
tiba nyingine zaidi ya KUSAME. Ni kitu cha kushangaza hata watu wadunia
wanataka kuwazidi akili baadhi ya watu wa Mungu. Katika accountance kuna kitu
kinaitwa Bad Debt Account. Yaani ni deni lililoshindikana kulipwa aidha kwa
kudhurumiwa au mdeni amekufa au kufirisika. Wahasibu hufungua account hiyo
ambayo ni ishara ya kusamehe deni lililoshindikana kulipwa, kisha wanafanya
mikakati mipya ya kusawazisha pengo hilo .
Sasa je! Kuna tatizo gani linalowafanya watu wa Mungu washindwe KUSAMEHE?
Nikifungua Biblia kwenye kitabu cha WAEFESO 4:26 Biblia inasema:
Nikifungua Biblia kwenye kitabu cha WAEFESO 4:26 Biblia inasema:
"Mwe na hasira, ila
msitende dhambi; jua lisichwe na UCHUNGU wenu bado haujawatoka." (Efe
4:26)
Unaona sasa; tatizo kubwa la
watu ni kuruhusu UCHUNGU KUWATAWALA. Tunapoambiwa "MWE NA HASIRA, ILA
MSITENDE DHAMBI.." Kumbe inawezekana kabisa mtu kupatwa na hasira kwa
sababu makwazo na majaribu ni mengi tuyapatayo kila siku, lakini tumeambiwa
“MWE NA HASIRA LAKINI MSITENDE DHAMBI”;
na tena tunaambiwa “...JUA LISIZAME TUKIWA BADO NA UCHUNGU NDANI YETU.” Tunalazimika
KUSAMEHE kwa ajili ya faida yetu sisi
wenyewe. Ndiyo maana tukisoma WAEFESO 4:26 imeandikwa: "wala msimpe
Ibilisi nafasi."
Hivyo basi, kumbe KUTAWALIWA NA UCHUNGU NI NJIA YA
KUMPA SHETANI NAFASI. Tunaposoma WAEFESO 5:17 tunaona imeandikwa:
"Kwa sababu hiyo msiwe
wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana". (Efe 5:17)
Bila shaka hadi hapo nimeeleweka
vizuri. Sasa basi; Athali ya tatu ya
KUTOKUSAMEHE ni kama ifuatavyo:
iii/: MUNGU HATAKUSAMEHE DHAMBI ZAKO.
KUTOSAMEHE ni moja ya sababu ya KUTOSAMEHEWA. Neno DHAMBI, lina maana ya kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Dhambi ni kuvunja amri/sheria za Mungu. Mtu atendapo DHAMBI anakuwa haumkosei mwanadamu bali umemkosea Mungu. Hivyo basi, ni Mungu pekee ndiye awezaye KUKUSAMEHE. Kwa hiyo, Mungu hawezi kukusamehe wakati wewe hautaki KUSAMEHE wenzako. Neno la Mungu linatuambia kwamba:
iii/: MUNGU HATAKUSAMEHE DHAMBI ZAKO.
KUTOSAMEHE ni moja ya sababu ya KUTOSAMEHEWA. Neno DHAMBI, lina maana ya kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Dhambi ni kuvunja amri/sheria za Mungu. Mtu atendapo DHAMBI anakuwa haumkosei mwanadamu bali umemkosea Mungu. Hivyo basi, ni Mungu pekee ndiye awezaye KUKUSAMEHE. Kwa hiyo, Mungu hawezi kukusamehe wakati wewe hautaki KUSAMEHE wenzako. Neno la Mungu linatuambia kwamba:
"Nanyi, kila msimamapo
na kusali, SAMEHENI, mkiwa na neno juu ya mtu; ILI NA BABA YENU ALIYE MBINGUNI
AWASAMEHE NA NINYI MAKOSA YENU." (Marko 11:25)
Tukizidi pia kusoma ule
mstari wa 26, tunaona Mungu anasisitiza kwa kusema:
"Lakini kama ninyi
hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu."
(Marko 11:26)
Mungu ametuweka wazi
kabisa; ENDAPO KAMA SISI HATUSAMEHE, VIVYO HIVYO NA SISI HATUTASAMEHEWA. Sasa
je! Ni nani asiyetenda makosa au kumkwaza mwenzake kwa namna yoyote ile? Bila
shaka hapa jawabu ni HAKUNA. Kila mmoja wetu umkwaza mwenzake kwa namna fulani
fulani. Kwa hiyo hatupaswi kuruhusu UCHUNGU ututawale hata kidogo ili Shetani
asipate nafasi ndani yetu. Kwa kuwa sote huwa tunakoseana, ni lazima
tusameheane ndipo na sisi tupate kusamehewa na Mungu.
Madhara mengine ya kutosamehe
ni haya yafuatayo:
iv/: MUNGU HAPOKEI SADAKA
ZAKO, NA WALA HAJIBU MAOMBI YAKO.
Nikifungua Biblia Takatifu
kwenye kitabu cha MATHAYO 5:23,24 tunaona pameandikwa kwamba:
"Basi ukileta sadaka
yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako,
kisha urudi uitoe sadaka yako."
Mungu huchukizwa na sadaka
za mwenye dhambi. Sadaka za mtu mwenye dhambi hazipokelewi mbele za Mungu.
Ndiyo maana imeandikwa kuwa utii ni bora kuliko dhabihu. Mungu si masikini hata
ababaishwe kwa sadaka zako. Tukisoma kitabu cha HOSEA 6:6 Mungu anasema:
"Maana nataka fadhili
wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka...",
Mungu hababaishwi na hako
kasadaka kako. Mungu si masikini hadi ababaishwe na uto tusadaka twako. Mungu
anapenda sadaka za mtu mwenye moyo safi ;
Ndiyo maana Biblia inasema kwenye MITHALI 21:3
"Kutenda haki na hukumu
humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka." (Mithali 21:3)
Mungu hupendezwa na moyo safi ; ndiyo maana amesema "...IACHE SADAKA YAKO MBELE
YA MADHABAHU, UENDE ZAKO, UPATANE KWANZA NA
NDUGU YAKO, KISHA URUDI UITOE SADAKA YAKO." Kwahiyo, usipopatana
(sameheana) na yule mliyekoseana, hakika Mungu hatapokea sadaka zako. Hivyo
basi, KUTOSAMEHE umfanya mtu kukosa kibali mbele za Mungu. Naunapokosa kibali
kwa Mungu maana yake unakuwa haujampendeza Mungu, vivyo hivyo kwa maana nyepesi
unakuwa umetenda dhambi, kwa maana dhambi ni kutenda kinyume na mapenzi ya
Mungu.
Hivyo basi, ninapenda
kuhitimisha somo hili kama ifuatavyo; Biblia
inasema kwenye kitabu cha WAEFESO 6:10,12
"Hatimaye, mzidi kuwa
hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu,
mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani."
Ninajua wapo watu ambao
watauliza; Je, silaha za Mungu ni zipi?
Silaha kubwa kabisa kuliko
zote ni NENO LA MUNGU lililomo ndani ya Biblia Takatifu; neno hilo la Mungu linapaswa kukaa kwa wingi ndani
yako. Neno la Mungu likikaa kwa wingi ndani yako, ukilifanyia kazi na
kulishika, ndipo Roho Mtakatifu atakaa ndani yako na kukuongoza namna ya
kufanya. Pasipo Neno la Mungu, hatuwezi kuyajua mapenzi ya Mungu. Kwahiyo,
silaha kuu ni NENO LA MUNGU. Ndiyo maana tukisoma WAEFESO 6:14-17 imeandikwa:
"Basi simameni, hali
mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu
utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani,
ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu..."
Sasa soma hapa kwa makini
zaidi, "...Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno
la Mungu."
Siku zote Shetani anataka
kuona watu wanapotea na kukosa baraka za Mungu. Shetani analeta majaribu na
makwazo mbalimbali ili watu waanguke na kuiacha njia ya uzima; Shetani anataka
watu wawe na uchungu ili wakose baraka za Mungu. Hauwezi kusema umemsamehe mtu
wakati bado unao uchungu moyoni mwako. Biblia inasema hakuna dhambi ndogo wala
dhambi kubwa, ni kwa sababu muongo na muuaji wote hukumu yao ni kutupwa kwenye ziwa la moto na kupata
humo mateso ya milele yote. Vivyo hivyo yeye asiyesamehe wenzake hukumu yake ni
ile ile kwenye ziwa la moto sawa sawa na muuaji.
Nikisoma WAEFESO 6:12 imeandikwa
Nikisoma WAEFESO 6:12 imeandikwa
"Kwa maana kushindana
kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya
wakuu wa giza
hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."
Ndugu zangu tuweni macho na
makini sana ,
Shetani hapendi kuona watu wanabarikiwa, hapendi kuona kazi ya Mungu inasonga
mbele, na hapendi kuona watu wanarithi uzima wa milele. SAMEHEANENI NA WALA
UCHUNGU USIKAE MIOYONI MWENU. Mwenyezi Mungu awabariki nyote mnaotendea kazi haya
mliyojifunza humu. Roho Mtakatifu awaongoze kwenye kweli yote, mbarikiwe katika
jina la Yesu Kristo. Amina.
0 MAONI:
Post a Comment