Wewe ni mungu mtoto wa Mungu.
TAMBUA & TUMIA MAMLAKA ULIYOPEWA.
Habari zenu miungu wenzangu, Hamjambo? Bila shaka mnao uzima tele katika jina la Yesu Kristo.
Kuna watu wameshituka niliposema: "Habari zenu miungu wenzangu." Je! Haujui kwamba wewe uliye ndani ya Kristo; wewe ni mungu mwana wa Mungu? Neno la Mungu linasema:
"You are gods, And all of you are children of the Most High." - PSALM / ZABURI 82:6 (NKJV)
au kwa Kiswahili maana yaka ni: "Ninyi ni miungu, Na ninyi nyote ni watoto wa Aliye Juu Sana."
Sisi ni "miungu" wakati Yesu ni "Mungu". Unapotaja neno "Mungu" kwa kuanzia herufi KUBWA ya mwanzo, yaani "M" unakuwa umemtaja Muumba; lakini ukianza na herufi ndogo ya kwanza, yaani, "m" hapo unakuwa umetaja viumbe.
Mimi ni "mungu" hata wewe pia ni "mungu". Bwana Yesu anasema:
"Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?" - YOHANA 10:34.
Sisi ni miungu kwa sababu Mungu anakaa ndani yetu; hivyo tumekuwa wana wa Mungu katika Kristo Yesu.
Sifa ya mungu mwana wa Mungu ni kutawala na kutumia mamlaka uliyopewa. Usimpe Shetani nafasi, yeye ni mdogo sana kwako. Wewe ndani yako umepewa Roho Mtakatifu ambaye ni Mungu akuongozaye. Ukiamini, kila nguvu za giza zitakutii na kukuogopa katika jina la Yesu Kristo. Hakuna pepo mchafu wala mtu mbaya atakayefanikiwa kukudhuru.
Bwana Yesu anasema:
"Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru." - LUKA 10:19
Wewe ni mungu mtoto wa Mungu (ZABURI 82:6) Tumia mamlaka uliyopewa katika jina la Yesu Kristo.
0 MAONI:
Post a Comment