KAMPENI YA UZIMA WA MILELE:
"KUTII NENO LA MUNGU NA UTAKATIFU KWANZA."Ukristo sio dhehebu; bali Ukristo ni mahusiano bora na Mungu.Watu wengi hudhani Ukristo ni dhehebu ambalo limeanzishwa ili kuleta ustaarabu fulani katika jamii. Wakristo wengi wanaishi maisha ya kuigiza kisa tu ni wafuasi wa kanisa fulani! Wengine wanayaacha maagizo ya Mungu na kuyaheshimu mapokeo potofu ya dhehebu fulani eti kisa tu na wao wanajiita wakristo! Wengi wanaishi maisha ya maigizo, wanatenda dhambi kwa siri huku wakijiita "wapendwa"! Ndugu yangu na rafiki yangu; hapo unajidanganya wewe mwenyewe. Hakuna dhambi unayoweza kumficha Mungu. Leo ninasema na roho yako! Yachunguze matendo yako, chunguza siri za nafsini mwako; umemtenda Mungu dhambi. Umekuwa mnafiki, umekuwa na majungu japo unajiita mkristo, umekuwa...
Sunday, December 28, 2014
Thursday, December 25, 2014
UKWELI KUHUSU CHIMBUKO LA SIKU KUU YA CHRISTMAS.!
UKWELI KUHUSU CHIMBUKO LA SIKU KUU YA CHRISTMAS.!
Tusiwe wanafiki, tusiwe waongo!
UONGO NI DHAMBI.
Mafundisho ya Yesu kazaliwa
tarehe 25 Disemba yametoka wapi? Christmas sio sikukuu ya kusheherekea tarehe
ambayo Yesu amezaliwa.
Tukitazama ushahidi wa Kibiblia
hauoneshi Yesu alizaliwa mwezi gani wala tarehe gani; hata pia tukitazama
ushahidi wa Kihistoria nao unatubainishia kuwa Yesu Kristo alizaliwa KATIKATI
YA MWAKA 6 kwenda wa 5 b.C. Hivyo basi Yesu Kristo alizaliwa miezi ya KATIKATI
YA MWAKA wala sio mwishoni mwa mwaka! Mambo haya ni muhimu sana kwako Mkristo
uelewe, sio unakwenda tu kama kipofu.
Kwa ushuhuda wa kweli, katika
Injili...